Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MARAIS wameendelea kumimini nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakauu wa Nchi za Afrika kuhusu nishati.
Marais waliowasili jana kwa ajili ya mkutano huo ni pamoja na Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu.
Rais huyo aliwasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Tinubu amelakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Tinubu yuko nchini kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaowakutanisha Viongozi wa Nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo.
Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, Â Mohamed Ould Ghazouani, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mohamed Ould Ghazouani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Festo Dugange,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 27 na 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.
Mkutano huo unawaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, wataalam wa nishati, viongozi wa sekta binafsi, na washirika wa maendeleo kwa ajili ya kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto za nishati na kuchangamkia fursa za bara hili.
Kipengele muhimu cha mkutano huu kitakuwa kupitishwa kwa Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya bara la Afrika.
More Stories
Tuzo za EAGMA zazinduliwa rasmi
Katibu Mkuu Nishati aipongeza Sweden kufadhili miradi ya umeme nchini
RAS Seneda akabidhi msaada wa Mablanketi kwa wazee na yatima