Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wassira, ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhakikisha ardhi ya vijiji iliyoporwa kinyume cha sheria, inarudishwa kwa wananchi.
Wasira alitoa maagizo hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho,waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM.

Amesema,watu wamejimilikisha ardhi kwa kutoa rushwa jambo ambalo CCM inakataa kwa nguvu zake zote.
“Haki ya Watanzania kumiliki ardhi ni sera ya msingi kwa CCM, kuna watu wanajimilikisha maeneo makubwa na hawayaendelezi kwa kutoa rushwa. Tunaomba maeneo yote ambayo yanamilikiwa kinyume cha sheria yarudishwe kwa wananchi,”amesisitiza.
“Watu wakipata matatizo sehemu yao sahihi ambayo wanaweza kupata ufumbuzi iwe CCM. Hivyo tunaendelea kuhamasisha kuwa kitu kimoja,hii ni muhimu hasa kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu, lazima tuungane ili tushinde kwa kishindo,”.


More Stories
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya
Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo