January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM ‘yawakuna’ wengi kwa kucheza kama Pele

Ni kwa kuwapitisha mapema Rais Samia, Mwinyi, Nchimbi kupeperusha bendera ya Chama, Dkt. Rweikiza, wadau, wamwaga pongezi

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar

WADAU mbalimbali akiwemo akiwemo Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dkt Jasson Rweikiza na Mbunge wa Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood, wamepongeza kuteuliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchaguwa na CCM kuwania.

Aidha wamepongeza Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa CCM. Aidha pongezi zingine zimetolewa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Akizungumza jana Mbunge Rweikiza alisema hatua ya chama chake kumteua mapema Rais Samia kuwa mgombea wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na na Dkt. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar ni sawa na kucheza kama Pele.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dkt. Rweikiza alisema Rais Samia anastahili miaka mitano tena kwa uchapakazi wake uliosababisha kuanza kufanyakazi kwa miradi yote ya kimkakati ikiwemo ya Reli ya Mwendokasi SGR na Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.

Dkt. Rweikiza pia alipongeza uteuzi wa Rais Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa urais Zanzibar kwani ndani ya miaka michache ya uongozi wake amefanya mambo makubwa ambayo yanamfanya kustahili mitano tena.

Alipongeza pia uteuzi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi katika nafasi ya mgombea mwenza kuwa ni turufu nyingine kwa CCM kwani ni mtu mwenye uzoefu wa kutosha, mwadilifu, mzalendo wa kweli na asiye na makuu.

“Nampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumleta Dkt. Nchimbi kuwa Makamu wa Rais kwasababu ni mtu ambaye uadilifu wake hauna mashaka kabisa… CCM imepanga safu bora kabisa nampongeza pia Makamu Mwenyekiti mteule ndugu Steven Wasira ambaye uzoefu wake ndani ya chama na serikali unaonekana dhahiri,” alisema

“Ndani ya muda mfupi ambao Dk. Nchimbi amekuwa Katibu Mkuu wa chama tumeshuhudia mageuzi makubwa sana ndani ya chama nampongeza sana Rais Samia kwa kumteua maana ni mtu mzoefu na mwadilifu sana,” alisema Dkt Rweikiza

Kwa upande wake Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepongeza viongozi hawa walioteuliwa na kuchaguliwa kwa nyadhifa hizo.

Taarifa ya TEF kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na kusainia na mwenyekiti, Deodatus Balile, ilieleza kwamba; “Matumaini yetu kama Jukwaa ni kuwa viongozi hawa wataendeleza jukumu
la kulitumikia taifa la Tanzania na kuwakomboa wananchi kutoka katika lindi la umaskini na kuwaletea maendeleo ya kweli.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao cha Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Katika mkutano huo Rais Samia na Rais Wazaziri Dkt. Hussein Ali Mwinyi, walipitishwa kwa asilimia 100 ya kura kuwa wagombea Urais wa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, huku Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiteuliwa kuwa mgombea mwenza.

Tunaamini viongozi hawa watakapopata nafasi kwa maana ya
kuchaguliwa wataendeleza utamaduni na jukumu la kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari bila vikwazo vya aina yoyote.

Kama alivyosema Rais Samia kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeongezeka nchini, tunatamani nchi yetu itanue wigo wa uhuru wa vyombo vya habari wananchi wapate kila taarifa kwa wakati ziwasaidie kufanya uamuzi wakiwa na taarifa sahihi.

Hongereni sana mlioteuliwa kwa nyadhifa hizo, tunatumaini Watanzania wakiwachagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mtaendeleza misingi imara ya nchi hii.”

Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood amempongeza Rais Samia, kwa kupitishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho.

Abood alimpongeza pia mgombea mwenza wa Rais Samia ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dtk. Nchimbi.

Akizungumza jana, Abood alisema kwa mambo makubwa aliyofanya Rais Samia alistahili alichofanyiwa na wanaCCM kwenye Mkutano Mkuu uliofanyika siku ya Jumamosi.

” Rais Samia ameifanyia nchi mambo makubwa sana anastahili mitano tena, nampongeza pia kwa kupata mgombea mwenza Dk Nchimbi ambaye naye ni mchapakazi na mtu mwenye uzalendo na nchi yake ambaye na ambaye amekifanyia mageuzi chama ndani ya muda mfupi aliokiongoza, Alisema Abood

Alimpongeza pia mgombea urais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na Makamu mwenyekiti wa CCM Steven Wasira kwa kuaminiwa kushika nafasi hiyo