Na George Mwigulu,Timesmajiraonline
,Katavi.
JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwaka mmoja limefanikiwa kudhibiti uharifu mbalimbali mkoani humo na kuwa chachu ya amani na usalama ambao umekuza sekta ya uchumi.
Kwa kipindi cha mwenzi Januari hadi Disemba, 2024 watuhumiwa 8064 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2023 ambapo watuhumiwa 7931 walikamatwa ikiwa pungufu ya asilimia 1.7 ya watuhumiwa 133.
Akitoa ripoti Januari 03, 2025 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi Kasta Ngonyani kwa Wanahabari amebainisha kuwa watuhumiwa waliokamatwa ni waliofanya makosa ya ukatili wa kijinsia,uvunjaji,wizi,mauaji,utapeli kwa njia ya mtandao,dawa za kulevya,pombe moshi na ukiukwaji wa sheria barabarani.
Akiwa katika ofisi za Jeshi hilo, Ngonyani ameweka wazi kuwa kesi zilizofikishwa mahakamani zilikuwa 4356 ambapo kesi 1870 zilipata mafanikio kwa washtakiwa kukutwa na hatia na kuhukumiwa.
“Watuhumiwa wameweza kuhukumiwa vifungo ikiwemo vya kunyongwa hadi kufa, vifungo vya maisha jela, miaka 30 na wengine vifungo vya nje huku kesi 176 zipo mahakamani zinaendelea kusikilizwa” Amesema
Kamanda huyo wa mkoa, Amefafanua katika doria na misako dhidi ya pombe moshi na madawa ya kulevya watuhumiwa 759 wakiwa na lita 10,674, watuhumiwa 285 wakiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi Kg 522 na gramu 689 walikamatwa.
Ngonyani ameendelea kusema kuwa watuhumiwa 54 wamauaji walikamatwa, watuhumiwa 42 wakiwa na silaha haramu ya gobole 29 zilikamatwa na risasi zake za gorori ambazo huzifanyia shughuli za uwindaji haramu.
“Tumefanikiwa kudhibiti wizi wa mifungo kwa kukamata watuhimiwa 48,watuhumiwa 21 tuliwakamata na nyara za serikali” Ameongeza huku akisema watuhumiwa 75 walikamatwa kwa kuingia nchini kinyume cha sheria na kwa upande wa usalama barabarani makosa 26,483 yalikamatwa.
Katika kutambua umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa wananchi, Kamanda huyo ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kutambua jukumu la ulinzi nila jamii yote hivyo ushirikiano ni mzuri ili kuweza kubaini, kuzuia na kutokomeza uhalifu kwa maendeleo ya mkoa.
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linaendelea na kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia hasa wa watoto kwa kutambua kuwa swala la ulinzi na usalama wa mtoto kupitia sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inasimamia huku wazazi na walezi waendelee kutoa huduma muhimu kwao.
More Stories
Mwinyi: Kuna ongezeko la wawekezaji Zanzibar
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi