Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
KWA kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba, mwaka huu idadi ya wageni zaidi ya milioni 1.9(1,943, 920), wameingia nchini ongezeko hilo likiwa limechangiwa na sekta ya utalii kupitia Filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Hayo yamebainishwa jijini Dar-es -Salaam jana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini, Dkt. Anna Makakala katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wahamaji nchini .
Amesema Tanzania imeendelea kufaidika na wahamiaji wanaoingia nchini kihalali kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi, kupitia watalii, wawekezaji, wafanyakazi wa kigeni, wanafunzi na wataalamu wa kigeni katika fani mbalimbali.
“Tanzania imekuwa ikipokea wahamaji kutoka mataifa mbalimbali, ambao wamekuwa wakiingia nchini kwa madhumuni ya kufanya shughuli za muda mfupi, au kuishi kwa muda mrefu,”amesema.
” Kundi hili ni chachu ya maendeleo kwa nchi yetu kwa vile wanachangia katika pato la taifa letu,”amesema.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha umoja na mshikamano kwa raia wa kigeni wanaoishi nchini kihalali bila kuwabagua kutokana na rangi, dini au mataifa yao.
Sanjari na hayo amesema Idara ya Uhamiaji inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi,kuwasimamia na kuwalinda vijana na mabinti wao hasa wenye umri mdogo na wa kati,ili wasirubuniwe na mawakala kwa ahadi za ajira au fursa za masomo nje ya nchi na hatimaye kuingizwa katika biashara ya usafirishaiji haramu wa binadamu, kwani biashara hiyo kwa sasa imeshamiri.
Dkt. Makalala ametoa wito kwa raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa nchi yetu kwa kuhakikisha wanaishi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji za nchi walizopo.
Wakati huo huo, Dkt. Makakala,amesema takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia Novemba mwaka ujumla ya vibali vya ukaazi 20,979 vimetolewa na Idara ya Huduma za Uhamiaji nchini kwa raia wa kigeni.
Awali akizugumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Charangwa Makwiro,amesema Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ilala ndio umekuwa ukiongoza kwa kupokea wahamiaji.
Aidha amesema zipo chagamoto mbalimbali ambazo zinakiwabili wahamiaji waliomaliza muda wao ikiwemo walio katika magereza ya Segerea na Ukonga hivyo ni muhimu kuangalia namna gani ya kuweza kuwasaidia kuondokana na chagamoto hiyo.
More Stories
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang