Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuzuia upotevu wa fedha za Serikali zaidi ya bilioni 583( 583,591,615,609.00), katika mshauri 162 yaliyokuwa katika hatua mbalimbali za michakato ya ununuzi wa umma kwa kipindi cha miaka takribani minne.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando,wakati akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa kongamano la 15 Wataalam wa Ununuzi Ugavi linaloendelea katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC),jijini Arusha.
“Katika kipindi cha takribani miaka minne tumeweza kusikiliza mashauri 162 na baada ya kupitia mashauri hayo, tumezuia zabuni 35 zenye takribani ya billioni 583.5,na endapo zabuni hizo zingetolewa kwa wazabuni hao waliokosa sifa kungeisababishia Serikali hasara katika eneo hilo,”amesema Sando.
Sando amesema, PPAA imekamilisha mchakato wa kujenga moduli ya kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki katika mfumo wa Ununuzi wa Umma Kieletroniki (NeST), kinachosubiriwa ni kukamilika kwa kanuni za rufaa za ununuzi wa umma ambapo zipo katika hatua ya mwishoni.
Ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa Kanuni Rufaa za Ununuzi wa Umma, PPAA itaendelea na programu ya mafunzo kwa wazabuni na taasisi za ununuzi mbalimbali kikanda ili kuwapa uelewa wa kutumia moduli hiyo wakati wa kuwasilisha malalamiko au rufaa kieletroniki.
“Tunategemea kuanza mafunzo ya kutumia moduli Kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita,na baadae kufuatiwa na mikoa mingine,” amesema Sando.
Awamu ya kwanza ya mafunzo ya kuhusu moduli ya uwasilishaji wa malalamiko/rufaa kwa njia ya kieletroniki yalikutanisha Mikoa ya Dar-es-Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani yalifanyika ,jijini Dar es Salaam tarehe 29 na 30 Mei 2024
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi