Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Sengerema
Taasisi ya Eagle Entertainment yampa tuzo ya heshima ya utawala bora Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kutambua mchango wake wa kuwaletea maendeleo wananchi.
Tuzo hiyo ya heshima ya Rais Samia imepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Senyi Ganga, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda,katika hafla ya utoaji tuzo za Eagle Entertainment Kanda ya Ziwa msimu wa nne,iliofanyika wilayani Sengerema ,Desemba 14,2024.
Mbali na Rais pia Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema,imepata tuzo ya heshima kutokana na utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo pamoja na usimamizi wa miradi hiyo.
Hata hivyo msanii wa muziki wa kitambo kidogo ambaye amewai kutamba na wimbo wa Mwanza zirekebishwe barabara Filbert Kabago kutokea kundi la BWV, amepata tuzo ya heshima kutokana na mchango wake katika jamii kupitia sanaa ya muziki.
Mkurugenzi wa Eagle Entertainment, Hassan Kuku,amesema sababu ya kumpatia tuzo hiyo Rais Samia,ni kutambua mchango wake katika kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya kimkakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Senyi Ganga,amesema jambo alilolifanya Mkurugenzi wa Eagle Entertainment,linatia moyo na la kupongezwa kama kijana, hivyo Serikali itaunga mkono tuzo za Eagle Entertainment ili adhima yakuanzishwa kwake ifikiwe.
“Tunaamini,mnapo tambua michango,mnasaidia pia kwa namna moja au nyingine,kuinua uchumi wa Tanzania.Kwa sababu hawa tunaowawezesha leo kwa makundi mbalimbali,katika maisha yao unaenda kuwafanya wajiamini na wajione kwamba wanaweza,”amesema Senyi.
“Tunashukuru kwa kutambua kazi anayofanya Rais,na ni kweli usiopingika amefanya kazi kubwa katika Wilaya yetu ya Sengerema,hakuna sekta ambayo imeachwa, hakuna sekta ambayo aina mradi unaotekelezwa,”amesema Senyi na kuongeza:
“Wilaya yetu ya Sengerema inakwenda kufunguka zaidi na tuna tegemea hata tuzo hizo zitakuwa kubwa,hivyo tunashukuru kwa kutambua mchango wake,”.
Sanjari na hayo,amesema vijana na wanasengerema,wajiandae na fursa ambazo ziakuja,ambapo daraja la kimkakati la Kigongo-Busisi maarufu J.P.Magufuli,ambalo litaifungua Wilaya hiyo.Pia na miradi mingine ikiwemo ya maji, barabara,afya na kilimo.
Ambapo jumla ya tuzo 32,zimetolewa katika msimu huu wa nne wa tuzo za Eagle Entertainment mwaka 2024,ikiwemo za wasanii, wajasiriamali, waandishi wa habari na waigizaji.
Kwa upande wa Waandishi wa habari,Daniel Limbe kutoka Sengerema amejinyakulia tuzo mbili ikiwemo ya Mwandishi bora wa habari za elimu pamoja na ukatili,huku Ibrahim Rojala akipata tuzo ya mwandishi bora wa habari za mazingira.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya