Na Penina Malundo,Timesmajira
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospital ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais kwenye Masuala ya Afya na Tiba, Prof. Mohamed Janabi, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi teknolojia za kisasa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Amesema maboresho yaliyofanywa na Rais Samia yamewezesha kufikia mafanikio hayo kwa kuhakikisha huduma bora za afya kutolewa.
Aliyasema leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa Salamu za Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa Watanzania, huku akiwataka kuzingatia mlo sahihi usiopitiliza ili kujiweka hatarini kupata Saratani.
Mbali na hilo,Prof.Janabi alisema muda sahihi ukifika atazungumzia suala la kugombea nafasi aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Dk. Ndugulile ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigamboni alifariki dunia Novemba 27, 2024 ikiwa ni miezi michache tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo.
Majibu hayo ya Profesa Janabi yanakuja ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Samia kumtaka kujiandaa kugombea nafasi hiyo huku akisema wamezipitia CV zaidi ya tano na kuona mkurugenzi huyo wa Muhimbili anafaa kuchukua nafasi ya Dk. Ndugulile muda utakapofika.
Prof. Janabi amesema ni sahihi Rais kupendekeza jina lake ila muda ukifika, WHO wakishatangaza na jina lake likapelekwa basi maswali yote yanayohusiana na jambo hilo atayajibu na kulizungumza jambo hilo.
“Kwa sababu vipi kama WHO hawatangaza, mimi naomba tuwe wavumilivu ndugu waandishi wa habari, ukifika muda sahihi mimi nina uhakika Serikali na mimi ni sehemu yake nitalijibu maswali yote yanayohusiana na suala hilo,”amesema Prof. Janabi
Akizungumzia ujumbe wake wa Chrismass na Mwaka mpya amesema ni muhimu jamii ikajikita kujikinga na magonjwa yasiambukiza kwa kuwa magonjwa hayo yanausumbufu na gharama kubwa kuyatibu.
Amesema takribani watu milioni 34.6 hufariki kila mwaka duniani kutokana na magonjwa yasiyoambukizwa kwa kuwa magonjwa ya moyo, shinikizo la damu ,kiharusi na magonjwa ya kisukari.
Amesema magonjwa ya moyo ,shinikizo la damu,kiharusi na ugonjwa wa kisukari huua asilimia 364 zaidi ya ugonjwa wa saratani kwa mwaka hivyo jamii inatakiwa kuweka msukumo wa kukabiliana magonjwa haya kutokana na madhara yake.
”Suluhisho la magonjwa haya ni kubadili mtindo wetu wa maisha kwa kulala sawasawa,kufanya mazoezi ,kuongeza mbogamboga ,matunda na kupunguza msongo wa mawazo .Na kwa kiasi kikubwa magonjwa hayo yanaathiri nchi hizi zinazoendelea.
Prof. Janabi amesema hajakataza watu kutokula, lakini anachoshauri watu kula kwa kiasi kula chakula bora kila mtu ana jukumu la kutengeneza utaratibu wake wa kula.
More Stories
Mavunde mgeni rasmi uzinduzi wa mnada wa madini ya vito Desemba 14,Mirerani
GST,BGS zafanya majadiliano namna ya kuanzisha mashirikiano katika tafiti na kujengeana uwezo
Utekelezaji wa Mou Tanzania,Burundi waanza rasmi