Na Mwandishi wetu,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan,amesema wakati dunia inaendelea na mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi,ipo haja kwa nchi wanachama kuwa na ajenda ya pamoja katika kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na matumzi ya nidhati safi.
Rais Samia aliyasema hayo katika Jukwaa lililowakutanisha viongozi wa mataifa yanayounda nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwemo wawakilishi wa baadhi ya mataifa hayo Jijini Arusha.
Lengo ni kutathmini changamoto,fursa na maendeleo kwa mataifa hayo ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Masuala haya ya mabadiliko ya tabianchi yana gharama kubwa kwenye nchi zetu. Kwa mfano Tanzania sisi tunatumia asilimia nne mpaka tano ya GDP yetu kwenye masuala ya kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi,” alisema Rais Samia.
Kimkakati mongoni mwa mambo ya msingi juu ya kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na kuwepo kwa soko la pamoja,kuondoa vikwazo kwa nchi hizo pamoja na kuwepo kwa sarafu ya pamoja.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo; “Kila nchi ilitamka kwamba ingependa kubakia na kumbukumbu yake, kuna alama na kama sisi tuna mwalimu Nyerere hatutaki kumpoteza, na Kenya wana Kenyata, hivyo mazungumzo bado yanaendelea,” alisema Balozi Kombo
Katika kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya hiyo baadhi ya wadau wakiwemo benki ya KCB imesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara hususani kwa wawekezaji na wafanya biashara kutoka mataifa hayo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono viongozi wa mataifa hayo.
More Stories
Wawili wadakwa na polisi tuhuma za kumuua Mwenyekiti UVCCM
Uganda yafurahishwa utendaji kazi,maabara ya GST na Masoko ya Madini
Mbibo apongeza mchango wa wajiolojia ,wanajiosayansi matumizi nishati safi