Na George Mwigulu,Timesmajiraonline,Katavi.
Mwanamziki wa kizazi kipya kutoka mkoa wa Katavi, Steven Kinyoto maarufu kwa jina la Chattaflyee ni mwanasheria ambaye ameamua kutimkia kwenye muziki wa kizazi kipya jambo ambalo limemfanya kuchaguliwa kwenye tuzo za Made in East Music and Media Awards.
Tuzo hizo hutolewa Nairobi nchini Kenya kwa wanamuziki wanaochipukia kwenye tasnia ya muziki ambapo wasanii mbalimbali wamefanikiwa kushinda tuzo hizo.
Chattaflyee akizungumza Novemba 26, 2024 amesema kufanya mziki ni sehemu ya kutimiza maisha ya ndoto zake bila kujali anapata changamoto gani ndani ya familia ambayo ilikuwa na matarajio ya kufanya kazi kupitia taaluma ya sheria.
Msanii huyo wa kizazi kipya ameweka wazi kuwa anawania tuzo kwenye vipengele viwili ambavyo ni video bora kupitia wimbo wa “Amazing” na wimbo bora wa “ Call me” ambapo kupitia tuzo hizo anaamini zitafungua fursa mpya kwenye mziki wake.
Vilevile amewaomba wananchi wa mkoa wa Katavi kuendelea kumpigia kura ambazo zitatamatika Decemba 05, 2024 kwani lengo lake ni kuendelea kupeperusha mkoa wa Katavi kupitia sanaa.
Bakari Hamza akimwakilisha Afisa utamaduni Mkoa wa Katavi amesema serikali itaendelea kutoa sapoti kwa wasanii wazawa kwa kuweka mazingira mazuri ya kuendesha sanaa ili kuweza kufikia maendeleo makubwa.
Ameeleza sanaa ni ajira kubwa kwa sasa nchini ambapo kama wasanii watafanya kazi kwa bidii kubwa na kwa kuzingatia ubunifu ndani ya sanaa hizo itakuwa rahisi kuonekana kwa jamii.
Aidha amehimiza wasanii wa mkoa wa Katavi kuhakikisha wanajisajili Balaza na Sanaa nchini BASATA ili kusaidia kazi zao kutambulika kisheria na kupata fursa zingine kubwa kutoka serikalini.
More Stories
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’