Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline.Dar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitakuwa na huruma na kiongozi atakayetumia madaraka yake vibaya kuwagandamiza na kuwaumiza wananchi.
CCM imesema katika kuhakikisha hilo watasimamia utendaji kazi wa viongozi hao, huku kikiwasisitiza kwenda kufanya kazi kwa kuwafanya wananchi hao kuwa kipaumbele chao wakati wote.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameeleza hayo leo Novemba 26, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbagala lililopo wilayani Temeke, Jijini Dar es salaam akifunga mikutano ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 utakaofanyika kesho Novemba 27, 2024.
Dkt.Nchimbi amesema, kwa kiongozi yeyote aliyeteuliwa na kupigiwa kura ajue kuwa wajibu wake mkubwa ni wananchi waliomchagua, hivyo kufanya mambo kinyume na kutimiza matakwa yao ni sawa na kupoteza imani kwa waliowaamini na kuwateua.
“Nasema hivi hatutakuwa na huruma na mgonbea wa CCM atayetumia madaraka yake kuwaumiza wananchi tunawategemeeni muwapende na kuwatumikia wnaanchi waliowachagua tofauti na hivyo tutapishana njia,”amesema Dkt.Nchimbi.
Aidha Dkt.Nchimbi amepongeza Wanaccm kufanya kampeni za amani na utulivu nchi nzima bila virugu, matusi wala mambo yoyote mabaya yasiyofaa.
Pia, amesisitiza wananchi kuendelea kusimama ‘kidete’ kukataa kufarakanishwa kwa maneno ya wana siasa huku akiwasisitiza kusimamia mambo yaliyo ya msingi yenye manufaa kwao na taifa kwa ujumla.
Alisema vyama mablimbali vya siasa vilijitokeza kuomba nafasi mbalimbali zinazowaniwa katika katika mitaa 80,400 nchi nzima na kusisitiza CCM imeweza kuweka watu 49,000 ambao ni sawa na asilimia 61 ya watanzania watakaopigiwa kura za ndio na hapana.
Aliongeza kwa wapinzani imekuwa pungufu ya kwao kwani waliweza watu takribani 30,000 tu.
Pia alisema wakati wa kupiga kura za maoni jumla ya watu 356,000 waliomba kupitishwa huku watu 80,000 walifanikiwa kupita lakini asilimia 99 ya walioshinda kura za maoni ndio walioteuliwa kuwania nafasi katika uchaguzi huo.
Aliongeza zaidi ya watu ambao hawakuteuliwa kulikuwa na sababu mbalimbali ikiwemo kutokukomaa kisiasa na wengine walipendwa sana na wananchi lakini hawakupata nafasi kwakuwa hawakujua kusoma na kuandika.
Alisisitiza kuwa mbali na watu zaidi ya 280,000 kutoteuliwa lakini wameonyesha ushirikiano mkubwa na kuwaunga mkono wenzao walioteuliwa kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi huo.
Alisema vyama vyote vya siasa vinatimiza jukumu la kidemokrasia kwenda kwenye uchaguzi lakini ni hiari ya mtanzania kuchagua chama kitakachoweza kuwawakilisha vizuri, kisichopenda ugomvi, kinatetea na kuona fahari kutumikia wananchi na kina kiu ya maendeleo.
Aidha Dkt.Nchimbi alisisitiza wanaccm kujizuia na kujiepusha na kuacha kugombana gombana kwani kunapoelekea chama kupoteza imani ya wananchi na kudharaulika hasa katika kipindi cha uchaguzi.
“Watanzania katika mikutano ya hadhara wanawez awakakupigia makofi lakini wakitoka wanaenda kusimuliana na kukudharau, wanakupigia makofi lakini kura wanakunyima,” alisema Dkt.Nchimbi.
Alisema CCM imepimwa vya kutosha na wananchi na wameona kuwa kinafaa kuwaongoza, hivyo amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
More Stories
Tanga kutumia vituo 5405,kupiga kura leo
NMB yatoa msaada wa vifaa Mufindi
Viongozi wa dini Katavi waomba wananchi kujitokeza kupiga kura