November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kufuatia uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika jana Mikoa yote nchini jana Novemba 20, 2024, kimeendelea kujizolea maelfu ya Wana-Chama kutoka vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA na kusema kuwa, hali hiyo inaashiria ushindi kwa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba 27, mwaka huu.

Akizungumza na maelfu ya watu katika Uwanja wa Mzimuni uliopo katika Kata ya Vijibweni, Wilaya ya Kigamboni, Jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM taifa, CPA. Amos Makalla amesema kuwa, hali hiyo ya wanachama kutoka vyama vya upinzani na kuhamia CCM ni ishara tosha ya Wana-Chama hao kutoendelea kuviamini vyama vyao.

Amesema, CCM kina imani ya kwenda kushinda katika uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, kwani Chama hicho kilijiandaa kwa kufanya maandalizi ya kutosha kwa kutumia fursa ya 4r za Mwenyekiti wa CCM Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.7

” Nilishasema tangu jana na bado naendelea kusisitiza kuwa, CCM tuna kila sababu ya kwenda kushinda katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27, kwani tulitumia vizuri fursa ya Rais Samia ya kuruhusu mikutano ya wazi kwa vyama vya siasa, hivyo tulizunguka Mikoa 20 nchi nzima kuelezea juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Wakati sisi tunazitumia fursa hiyo kuzunguka kila Mkoa kukiimarisha chama, wenzetu walikuwa wana hamasisha maandamano! na sasa hivi ndiyo wanakumbuka shuka kumekucha.. wale hawajajipanga bado kwa uchaguzi hivyo tunaomba muendelee kukiamini CCM ndiyo Chama ambacho kinadhamana na kitaendelea kuwaletea maendeleo”, amesema Makalla.

Aidha ameendelea kuwatoa hofu wananchi na Wana-Chama wa CCM kuendelea kukiamini chama hicho na kusema kuwa, kimewateua wagombea wenye sifa ya kukubalima kwa jamii na wataenda kuwaletea maendeleo