Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan zamemuelekeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo
la Kariakoo.
Rais Dkt. Samia alitoa maelekezo hayo jana wakati akizungumza kwa njia ya simu na Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na kusema:
“Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo.
Binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwa nusur ndug zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo.
Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la nokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hao,” alisema.
Aidha, Rais Dkt. Samia pia ameongeza kusema kuwa: “Kwa vikosi yetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa
maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana.
Wameonesha utu, uzalendo mkubwa na chapakazi wa hali ya juu sana.
Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu”
Rais Dkt. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.
More Stories
Washauriwa kuwa na subira hospitalini wanapojifungua watoto kabla ya wakati
Issa Gavu atua Geita kuzindua kampeni leo
Rais Samia ayapa ushauri Mataifa ya G20