September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

WASHTAKIWA waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya,  jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hukumu  hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma leo baada ya kuwatia hatiani kwenye mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Washtakiwa  ambao kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii wakati wakifanya unyama huo wakidai wametumwa na afande walikuwa wanakabiliwa na  kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Pamoja na hukumu  Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya sh. milioni moja