September 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uwekezaji mkubwa wa Samia kwa Wizara ya Afya umesogeza huduma bora kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Afya ina dhamana ya kusimamia utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wote ili kuwa na Jamii yenye afya bora na Ustawi, ambayo itachangia kikamilifu katika maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Kwa kutambua jukumu hilo, Wizara katika kipindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu
Hassan, imepatiwa kiasi cha sh. trilion 6.722 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele mbalimbali ili kuimarisha huduma za afya nchini.

Fedha hizo, amezitoa kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, ambapo Wizara ya Afya imetekeleza kwa mafanikio makubwa majukumu yake, ikijikita katika maeneo makuu mbalimbal yakiwemo; ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini,
kuimarisha upatikanaji wa dawa na bidhaa nyingine za afya, upatikanaji wa
huduma za ubingwa na ubingwa Bobezi nchini, kuimarisha huduma za
uchunguzi wa magonjwa ikiwemo huduma za mionzi, kuimarisha huduma za afya
ya Uzazi, Mama na Mtoto.

Maeneo mengine ni kudhibiti maambukizi ya UKIMWI, kifua kikuu, malaria
na magonjwa ya mlipuko, ajira kwa watumishi na ufadhili wa wanafunzi katika
ngazi na fani mbalimbali pamoja na kupitishwa kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa
wote.

Katika makala haya, Mwandishi Wetu anaeleza machache kati ya mengi zaidi yaliyofanywa na Rais Samia kutokana na maono, utu na mapenzi mema ya kutaka kuona wananchi wake wanakuwa na afya njema.

Rais Samia amefanyika uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kutolea huduma za afya ambapo vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 8,549 mwaka 2021 hadi kufikia vituo 9,610 Machi 2024.

Hii ni sawa na ongezeko la vituo 1,061. Lakini pia amefanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ambapo Serikali yake imejenga na kufanya maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maengo mapya, ukarabati na kukamilisha ujenzi wa hospitali mpya katika mikoa mipya mitano.

Maboresho hayo yamegharimu jumla ya sh. Trilioni 1.02 na yalifanyika
katika maeneo yafuatayo;

Moja, kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda
ya Kusini Mtwara na kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali
ya Rufaa ya Kanda Chato.

Hospitali hizi za Rufaa za Kanda zimeanza kutoa huduma katika miaka mitatu ya Uongozi wake. Pili, ameweza kuendeleza ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa mipya mitano
ambazo ni Katavi, Njombe, Songwe, Simiyu, Geita.

Hospitali hizi zimeanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo husika. Tatu, ameweza kuhamisha Hospitali nne kutoka majengo yake ya zamani kwa kujenga hospitali mpya katika maeneo mapya, hospitali hizo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Singida, Mara na Ruvuma.

Nne, Rais Samia ameweza kukarabati na kujenga majengo mapya ya kutolea huduma za afya katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Ligula (Mtwara), Sekoutoure (Mwanza),
Maweni (Kigoma), Sumbawanga (Rukwa) na Kitete (Tabora).

Tano, amewezesha ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na Hospitali za Halmashauri katika
maeneo mbalimbali nchini kama ilivyoonyeshwa na OR-TAMISEMI. Sita, amefanya ujenzi wa mitambo 21 ya kuzalisha hewa tiba ya oksijeni kwa ajili ya wagonjwa mahututi na wagonjwa wa dharura.

Kimsingi ongezeko la vituo vya kutoa huduma za afya nchini na maboresho ya miundombinu yaliyofanyika yametuwezesha kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi kama tunavyoelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

Hivi sasa asilimia 80 ya wananchi wanapata huduma za afya ndani ya kilometa tano ya maeneo yao wanayoishi, ambapo lengo ni kufikia asilimia 95 ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wa kuimarisha huduma za ugunguzi wa magonjwa katika kuimarisha hizo, Serikali yake imenunua vifaa Tiba vya Uchunguzi na matibabu ya wagonjwa vyenye
thamani ya sh. bilioni 290.9 ambavyo vinapatikana kuanzia ngazi ya Hospitali
ya Taifa hadi Hospitali za Rufaa za Mikoa (RRHs) na Halmashauri.

Hivi sasa huduma za kipimo cha CT Scan sasa zinapatikana katika Hospitali 27 kati ya
Hospitalii 28 za rufaa za Mikoa nchini.

Kwa mwaka 2023, jumla ya wagonjwa 15,386 walipatiwa huduma za kipimo cha CT Scan katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambapo huduma hizo zilikuwa hazitolewi katika hospitali za Rufaa za Mikoa hapo awali.

Aidha, idadi ya vitanda vya wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini
imeongezeka kutoka vitanda 86,131 mwaka 2021 hadi vitanda 126,209 Machi

  1. Ongezeko la vitanda vya wagonjwa limesaidia kuongeza ubora na ufanisi wa huduma za afya hususani huduma za afya ya mama na mtoto.

Vilevile Serikali imekamilisha ujenzi wa wodi 45 za wagonjwa mahututi (ICU)
katika hospitali ngazi ya Taifa, Maalum, Kanda na Mkoa na kuziwekea vifaa na
vifaa tiba.

Pia Serikali inaendelea na ujenzi wa ICU 28 katika ngazi ya Halmashauri ambapo 27 kati ya hizo zimekamilika na moja (1) iko hatua ya ukamilishaji. Hatua hii imeongeza idadi ya vitanda kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) katika vituo vya umma kutoka vitanda 258 vya mwaka 2021 hadi kufikia vitanda 1,362 mwaka 2023.

Ongezeko la vitanda vya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali za umma linalenga kusogeza huduma karibu na wananchi, kupunguza rufaa za wagonjwa wanaohitaji huduma za ICU kwenda katika Hospitali za Rufaa za Mikoa 4 na Taifa na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa sambamba na kupunguza vifo vinavyotokea ndani ya hospitali ambavyo vinaweza kuzuilika kati ya asilimia 20 hadi 30.

Eneo lingine ni kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa na bidhaa za afya ambapo, katika kipindi cha miaka mitatu, wastani wa sh. Bilioni 20 zimekuwa zikitolewa kila mwezi.
Upatikanaji wa fedha hizo umewezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawa muhimu na bidhaa nyingine za afya (aina 290) katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kufikia asilimia 84 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 58 mwaka 2022.

Pia , katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Machi 2024, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza katika huduma za afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.

Uwekezaji huo umefanyika katika maeneo yafuatayo ya ukamilisha ujenzi wa jengo la kutoa huduma za afya ya Mama na Mtoto Meta iliyopo katika Jiji la Mbeya ambayo tayari inatumika na imegharimu sh. bilioni 13.2.

Nyingine ni kuendelea na ujenzi wa majengo ya huduma za Mama na Mtoto
(Maternity Blocks) kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa ambazo ni Sekou Toure (Mwanza), Geita, Simiyu, Mawenzi, Njombe na Songwe ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 71.1.

Pia, Serikali ya Awamu ya sita imeimarisha huduma za upasuaji wa wajawazito kwa kuongeza vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni (CEMoNC) kutoka vituo 340 mwaka 2021 hadi kufikia vituo 523
mwaka 2023.

Pua imeanzisha wodi maalum kwa ajili ya huduma za watoto wachanga wagonjwa (Neonatal Care Units – NCU), ambapo hadi kufikia Desemba 2023 jumla ya Hospitali 189 zinatoa huduma za NCU ikilinganishwa na Hospitali 165 mwaka 2022 na Hospitali 14 tu mwaka 2018.

Imeimarisha upatikanaji wa bidhaa za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ambapo upatikanaji wake katika Vituo vinavyomilikiwa na Serikali umeongezeka kutoka asilimia 82.5 mwaka 2021 hadi asilimia 88.2 mwaka 2023.

Imeimarisha huduma za Saratani ya mlango wa kizazi, ambapo jumla ya mashine 140 (Thermalcoagulator) za uchunguzi wa Saratani zimenunuliwa na kusambazwa kwenye vituo 140 vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri 104 katika Mikoa 26. Vifaa hivi vina thamani ya jumla ya shilingi Bilioni 1.1.

Serikali ya Awamu ya Sita imeanzisha mfumo wa kieletroniki wa M-mama unaoratibu rufaa, kwa kusafirisha akina mama wajawazito na watoto wachanga wanaohitaji huduma za dharura kutoka ngazi ya jamii hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya au kutoka
kwenye kituo cha kutolea huduma cha ngazi ya chini kwenda kituo cha
ngazi ya juu.

Kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi mwaka 2023 mfumo huu umendelea kufanya kazi katika Mikoa yote 31 Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, jumla ya wateja 46,941 wamenufaika na huduma za dharura za rufaa, kati ya hao akina mama walikuwa 38,560 sawa asilimia 82, watoto wachanga walikuwa 8,273 sawa na asilmia 17 na mama
pamoja na mtoto kwa pamoja walikuwa 108 sawa na asilimia moja.

Vilevile, wateja wote wa M-mama wanahudumiwa na watoa huduma waliopo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali nchini. Mfumo huu umerahisisha utoaji wa huduma za dharura kwa wakati kwa kuwafikisha wateja katika vituo sahihi vya matibabu.

***MATOKEO

Kutokana na. uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hasssan katika kuimarisha ubora wa huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ambapo kupitia Viashiria vikuu vinavyotumika kupima mwenendo wa ubora wa huduma kwa Nchi Wanachama wa Shirika la Afya Duniani imejidhihirisha wazi kuwa Nchi yetu imefanya vizuri sana katika kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto katika kipindi cha miaka mitatu.

Matokeo ya baadhi ya viashiria hivyo ni pamoja ongezeko la wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Idadi ya wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeendelea kuongezeka kutoka asilimia 63 mwaka 2021 hadi asilimia 85 waka 2023.

Lengo la nchi ni kufikia asilimia 95 ya wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ifikapo mwaka 2030. Serikali imepunguza vifo vya wanawake wajawazito kwa asilimia 80 .

Aidha, imeweza kuimarisha huduma za uzazi, mama na mtoto kumepelekea kupunguza vifo vya wajawazito vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa sasa .

Vifo vya watoto umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2022.

Vifo vya watoto umri chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka vifo
43 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 33 kwa kila
vizazi hai 1,000 hadi sasa,

Vifo vya watoto wachanga (wenye umri wa chini ya siku 28) vimepungua kutoka 25 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi vifo 24 kwa vizazi hai 1,000 hadi sasa.

Mwishoooooooooo