Na Joyce Kasiki,Tomesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Nanyamba Abdallah Chikota ameihoji Serikali lini itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Nyundo
Chikota ameuliza swali hilo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.
Amesema kituo hicho kimejengwa kwa nguvu za wananchi na kwamba konahitaji fedha kwa ajili ya kumalozia ujenzi.
Akijibu swali hilo,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Festo Dugange amesema Kituo cha Afya Nyundo kilichopo katika Mji wa Nanyamba kilianza
kujengwa kwa nguvu za wananchi.
Amesema , Septemba, 2023 Halmashauri kupitia shirika la Mafuta Tanzania (TPDC) ilipokea kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma kwa wagonjwa wa nje – OPD.
Dugange amesema , katika mwaka 2023/24, Shirika la TPDC limetoa shilingi milioni 360 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kutolea huduma kwa wagonjwa wa nje katika kituo hicho na kuanza kujenga miundombinu mingine inayopungua ikiwemo jengo la wazazi lenye huduma za upasuaji wa dharura.
Kwa mujibu wa Dugange ,Ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa wa nje uko asilimia 70, na majengo mengine yapo hatua ya kuandaa eneo la ujenzi na kazi zinaendelea.
More Stories
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang