Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Morogoro
KAMPUNI ya sukari ya Kilombero ambayo ilishiriki maonesho ya NaneNane mwaka huu,yaliofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 katika mikoa ya Dodoma na Morogoro, imewataka wakulima kuchangamkia fursa katika upanuzi wa Kiwanda cha K4.
Nane Nane hutumika kama kitovu cha wakulima na umma katika kuangazia maendeleo katika kilimo. Ushiriki wa kampuni ya sukari Kilombero unaonesha kujitolea kwake kusaidia na kuinua jamii ya wakulima nchini Tanzania.
Upanuzi wa kiwanda cha K4 ambao unatazamiwa kukamilika ifikapo Juni 2025, utaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa uzalishaji wa sukari.
Mradi huo unalenga kukidhi ongezeko la mahitaji ya sukari huku ukitengeneza fursa nyingi kwa wakulima wa ndani.
Kiwanda cha K4 kitaiwezesha kampuni hiyo kupata miwa zaidi kutoka kwa wakulima, hivyo kuongeza kipato chao na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya kikanda.
Akizungumza katika mahojiano na wanahabari mjini Dodoma, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Wadau wa kampuni hiyo Victor Byemelwa, amesisitiza umuhimu wa mpango huo.
“Nane Nane ni jukwaa muhimu kwetu kwani ni fursa ya kuungana na wakulima na kujua changamoto mbalimbali, tunaendelea kuwasititiza kuchangamkia fursa zitakazotokana na upanuzi wa kiwanda cha K4,” amesema Byemelwa.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa