Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Mwanza
Miili ya watu wawili kati ya watano ambao walikuwa hawajapatikana baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria imeopolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano wa wananchi wa Wilaya ya Sengerema mkoani hapa.
Mtumbwi huo uliokuwa umebeba watu zaidi ya 20, ulizama Agosti 05,2024 majira ya 2:00 usiku katikati ya Kisiwa cha Yozu na Ziragula wakati wakitokea kwenye sherehe ya mashabiki wa Yanga (Yanga day) iliyofanyika kisiwani Yozu wakielekea kitongoji cha Itabagumba ambapo watu 17 waliokolewa.
Agosti 07.2024 majira ya saa 5 asubuhi (11:00hrs) eneo la Butala Mawe mawili, kisiwa cha Yozu, Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kuopoa miili ya watu wawili ambao ni Mashauri Ishabakaki(42), mkazi wa Mbugani na Jonathan
Mutasyoba(50) .
Akizungumza mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa jitihada za kutafuta watu wengine watatu zinaendelea ambao ni Masaka Angote(60) mkazi wa Burihaeke, Edward Kachelemi(46), mkazi wa Burihaeke na Shija Paschal(30) mkazi wa Yozu ambao bado hawajapatikana.
 “Miili ya marehemu waliopatikana imekabidhiwa kwa ndugu kuendelea na taratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu,”ameeleza DCP Mutafungwa.
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi