Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza
WATANZANIA wameaswa kuchangamkia fursa, kuthamini na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na sekta za serikali kupitia maonesho ya Wakulima (Nane Nane) ili kuona nchi ilipofikia kiuchumi,kijamii na kiimani.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke,amesema hayo leo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika kikanda uwanja wa Nyamh’ongolo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani hapa.
Amesema monesho ya Nanenane yanayofanyika jijini Mwanza,ni fursa kwa wananchi wa imani na dini mbalimbali na si ya wakulima na wafugaji pekee,hivyo wayathamini kwa kutembelea mabanda wakajifunze na kuona.
Sheikh Kabeke amesema kutokana na fursa zilizopo serikali katika maonesho ya mwaka huu, imetoa fursa kwa taasisi za dini kuonesha kazi zinazofanyika katika jamii, hivyo ni fursa kwa wananchi kutembelea mabanda hayo wajifunze na kupata elimu ya mambo mbalimbali.
Pia amewakumbusha Watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo nchini tunapoelekea katika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa.
“Niwasihi tuendelee kulinda amani na utulivu wa nchi yetu, hata maonesho haya ya Nane Nane yanayofanyika ni ushahidi wa utulivu mkubwa uliopo,hivyo tukiudumisha tutaona faida za utulivu huo,”amesema.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi