Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
UMOJA wa Wanawake Kata ya Kimara Wilaya ya Ubungo, chini ya Mwenyekiti wake Mwajuma Ramadhani, wamefanya kikao Chake cha Baraza la Kikanuni kwa lengo la kuendelea mikakati ya Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa.
Katika kikao hicho kilichofanyika Julai 28 mwaka huu mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti CCM Kata ya Kimara, Bosco Bugali akiongozana na Diwani wa Kata hiyo Arch. Ismail Mvungi na Diwani viti Maalum, Nuru Mbezi.
Agenda Kuu katika Baraza hilo ni kuendelea na mikakati kulelekea katika chaguzi za Serikali ya Mitaa.
Akizungumza katika kikao hicho mgeni rasmi, Bosco Bugali aliwaelezea Wajumbe wa Baraza hilo mambo mengi ya kuyaishi na kuyaendea katika Maisha binafsi na Siasa ili kuimarisha CCM.
Licha ya Mipango mikakati ya uchaguzi, Diwani waKata ya Kimara aliwapongeza wajumbe wa Baraza hilo kwa mikutano mikuu ya matawi yaliyofanyika kwa mafanikio makubwa.
Hata hivyo Diwani huyo hakuacha kuwapa zawadi viongozi wote wa Baraza hilo, kwani siku zote Mcheza Kwao hutunzwa.



More Stories
Rais Samia atoa msaada kwa kituo kinachohifadhi wasichana waliokimbia ukatili
Mo Dewji na Urithi anaoujenga ,unavyoenda mbali zaidi ya mafanikio binafsi
Mulika Community kusaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili