Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watanzania kuacha kutoa taarifa zao binafsi kwenye mitandao ya kijamii kwani duniani imeharibika.
Amesema wao kama viongozi wanaendelea kufanya wajibu wa kuhakikisha wanathibiti tabia hizo ambazo zimekuwa zikifanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mhandisi Mahundi amesema hayo Julai 12,2024 wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha CUom kilichopo jijini Mbeya.
“Mimi na wewe lazima tuthibiti pamoja, tunza taarifa zako usimpe mtu yeyote na usimwamini mtu leo mpo kwenye urafiki kesho mkikosana amezipeleka halafu inakuja kuleta shida,”amesema Mhandisi Mahundi.
Aidha Mhandisi Mahundi amesema wao kama Wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari miezi miwili iliyopita Rais Samia alizindua taasisi ya kutunza taarifa za mtu binafsi lakini bado kuna watu watukutu mtaani wa kukopesha fedha ndogo ndogo kuanzia sh.100,000 kushuka chini mtu akichelewa kulipa zinaanza kutumiwa jumbe za vitisho kwa watu waliopo kwenye simu ya mkopaji .
“Pametokea ombwe kubwa sana mitaani la kukopesha fedha ndogo ndogo mkopaji akichelewa tu wale watu waliopo kwenye simu ya mkopaji wanaanza kutumiwa sms za vitisho kuwa bwana David alikopa kiasi fulani cha fedha na kuwa wewe ni mmoja wa wadhamini wake sababu tu mnawasiliana mara kwa mara na wakati huo David anakopa hakukuwa na mawasiliano yeyote mwisho wa siku unakuta unapigwa picha bila kujijua,”amesema Mhandisi M
Pia amesema Wizara hiyo wanashirikiana na Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha “Cirber” kushughulikia changamoto hiyo kwa kutoa matangazo kwa wananchi kuwa makini na taarifa zao binafsi kuacha kutoa ovyo.
“Huko mnako cheza cheza kwenye mitandao ya kijamii msiweke taarifa zenu binafsi na msipende kuandika onyo mfano Facebook, Twitter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii Dunia imeharibika hivi sasa umakini ni muhimu,”amesema.
Baadhi ya wanachuo walioshiriki mkutano huo wamesema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa changamoto kubwa na baadhi ya vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikipitia huko .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi