September 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PURA kuongeza wawekezaji kwenye Gesi Asilia

Na Penina Malundo,Timesmajira

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka ya  Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),Halfani Halfani,amesema mamlaka yao itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye maeneo yaliyo wazi ili  kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani .

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba Jijini Dar es salaam, Halfani amesema PURA ina majukumu ya kusimamia na kudhibiti shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli.

Amesema hadi sasa kuna mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwenye gesi asilia,ikiwemo kuchangia kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, kupitia majumbani na kwenye magari.

Amesema watanzania zaidi ya 1,428 wamepata ajira za kudumu na za muda katika miradi ya ufatiliaji wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini “Kuanzishwa Kwa kazidata ya watoa huduma wa kitanzania ambapo Kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa”. amesema

Halfani na kuongeza sh. Billioni 173 zimeokolewa kupitia kaguzi za mikataba ya uzalishaji na ugawaji wa mapatoAmesema kwa muda mrefu wamekuwa hawana wawekezaji wa kutosha hivyo PURA itahakikisha  inaongeza wawekezaji hao katika maeneo ambayo yapo wazi.

Aidha ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kusimamia na kuyawezesha maonesho haya na kuwa na hadhi ya kimataifa.

”Miaka ya nyuma maonesho haya kwa kusema kweli  yalikuwa kama gulio lakini kwa sasa yameboreshwa na kuwa na hadhi ya Kimataifa,naipongeza Tantrade kwa hatua kubwa iliyopigwa “.amesema