October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mifumo ya TEHAMA itaongeza uwazi zaidi kwenye utoaji huduma- Waziri Ndejembi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema utoaji huduma kupitia mtandao sio tu unaongeza ufanisi lakini pia unaongeza uwazi zadi.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo baada ya kupatiwa maelezo ya huduma ya PSSSF Kidigitali, ambapo mwanachama kupitia Application ya PSSSF Kiganjani Mobile App, anaweza kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake katika Mfuko, wakati alipotembeela banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam Julai 7, 2024.

“Matumizi ya Tehama inamuwezesha mwanachama kuona michango yake tangu alipoajiriwa, anaona amechangia kiasi gani, mwajiri wake ameleta kiasi gani, matumzii haya yanaleta uwazi mkuwba sana kwa jamii nzima inayocvhangia kwenye Mfuko.” Alifafanua.

Alisema, kustaafu si jambo la dharura, kila mtu anafahamu ifikapo miaka 55 kwa hiari na 60 kwa mujibu wa sharia, ni vema mtu akajiandaa mapema.

“Kwa kuweka APP ya PSSSF Kiganjani itasaidia kuondokana na changamoto hiyo.” Alisisitiza.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razak Badru amesema, Maonesho hayo yamewawezesha kuwahudumia wanachama wa Mfuko ambao wameweza kuoa michango yao, lakini pia kupata elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani.

“Baadhi ya wanachama wanakwenda katika baadhi ya shughuli ambazo mMfuko umekwua ukifanya kwenye maonesho hayo.” Alifafanua.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa ametoa wito kwa wanachama kutumia simu janza kupata huduma zinazohusiana na uanachama wao kwa njia rahisi.

“Wito wangu kwenye swala hili, wanachama wetu tutumie hizi simu ambazo tunazo sio tu kwa kupiga simu au kutuma ujumbe, tumia simu yako kupata huduma za Mfuko na muda mwingine utumie kufanya shughuli za uzalishaji mali.” Alisema.

Nate Mwanachama wa PSSSF, Bw. Ricky Sambu, yeye amepongeza Mfuko kwa hatua hii ya kufanya maboresho ya utoaji huduma.

“Kupitia PSSSF Kiganjani inanisaidia kuona michango yangu ya kila mwezi na hata ikitokea kuna pengo ninamuona HR, ninawapongeza PSSSF kwa kutupatia elimu ya kutumia huduma hii.” Alisema.