October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi lakamata watu saba, wakiwemo watumishi wa CRDB

Na Patrick Mabula , Kahama.

Watu saba wakiwemo watumishi watatu wa benki ya CRDB tawi la Kahama wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma ya wizi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 305 toka kwenye akauti za wateja.

Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga , Kenedy Mgani amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa 8 mchana baada ya kuwekwa mtego wa polisi.

Mgani amesema watu hao 4 ni kutoka jijini Dar-es-Salaam majina yao yamehifadhiwa ambapo wafika katika benki hiyo kuchukua fedha hiyo katika akauti za wateja wa benki hiyo.

Amesema katika mpango huo kati ya watu hao waliingia katika benki hiyo na kwenda kwa meneja huduma kwa wateja wa benki hiyo aliwasikiliza na kisha kuwaagiza watumishi wengine wawili kuwahudumia .

Mgani amesema ndipo walipoanza kuwahudumia na kutoa kutoa kwanza kiasi cha shilingi 30 milioni kwa kutumia kadi bandia kwa moja ya akaunti ya wateja na baadae walitoa kiasi cha shilingi 275 ndipo walipokamatwa kutokana na mtego ulikuwa umewekwa na polisi.

Amesema watu toka Jijini Dar-es-Salaam ni mtandao wa wizi kwa njia hiyo ambapo majina yao yamehifadhiwa na jeshi la polisi linaendelea kuwatafua wengine wa kundi hilo.

Kaimu kamanda ,Mgani ametoa wito kwa wateja wa Mabenki kuwa na tabia ya kukagua mala kwa mala taarifa za fedha zao kwenye akauti zao.