November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la polisi laitikia uvushaji wa wanafunzi barabarani

Picha wa msaada wa wa Mtandaoni ikionesha wanafunzi wakiwavusha wenzao wa kusimamisha magari kwa kutumia vifaa vya usalama barabarani chini ya usimamizi wa askari polisi.

Joyce Kasiki

BAADA ya wananchi kuliomba Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kuwapa mafunzo ya usalama barabarani wanafunzi wakubwa wanaosoma katika shule ya  msingi Mlezi kata ya Hazina mkoani Dodoma  ili waweze kuwavusha wenzao barabara wanapoingia shuleni,jeshi hilo tayari limetimiza ahadi yake ambapo wanafunzi hao sasa huwavusha wenzao kwa kutumia alama za usalama barabarani.

Awali watoto wa shule hiyo hasa wadogo wenye umri wa chini ya miaka minane walipata adha ya kuvuka eneo hilo na ilikuwa hatari kwa ulinzi na usalama wao wawapo shuleni.

Licha ya eneo hilo la barabara kubwa inayotoka hospitali ya Taifa ya magonjwa ya Akili Mirembe kuelekea Kanisa Kuu la Roma kuwa na kivuko cha watembea kwa miguu maarufu pundamilia,lakini kivuko hicho kimefutika na hivyo magari kupita kwa mwendo kasi katika eneo hilo la shule kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wa watoto wanaosma shuleni hapo.

Hatua hiyo ilikuwa inahatarisha ulinzi na usalama wa watoto ambao wakati mwingine hupata ajali katika barabara hiyo.

Baadhi ya wananchi wamelipongeza Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kwa mwitikio huo ambao angalau unawahakikishia watoto ulinzi na usalama kwa mustakabali wa ukuaji wao.

George Mazengo mkazi wa mtaa wa Hazina anasema hatua hiyo ya wanafunzi kuvusha wenzao ni nzuri kwa usalama wa wanafunzi wanaotumia kivuko hicho hasa wale wadogo.

Hata hivyo analiomba jeshi hilo kuimarisha suala la mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi shuleni hapo ili wawe na uaasiri wa kusimamisha magari na kuwavusha wenzao.

“Kweli wanafunzi tunawaona barabarani wakiwa na vifaa vya usalama barabarani wakisimamisha magari lakini zoezi hilo limekuwa likisuasua sana,inawezekana wanafunzi ahawajapata mafunzo ya kutosha.”anasema Khamis

Aidha analiomba Jeshi hilo kuanzisha klabu za usalama barabarani ili wanafunzi wawe wanapata mafunzo ya mara kwa mara na hivyo kuwawezesha kufanyaazi hiyo wa ufanisi zaidi,

Vile vile ameliomba jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kuwaalika wanafunzi hao wenye maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa lengo la kuendelea kuwajengea uzoefu masuala ya usalama barabarani.

Angelina Gerald mkazi wa mtaa huo anasema”hivi ni shule ya msingi ambayo Ina watoto wale wadogo wanaosoma chekechekea’darasa la awali’,dararasa la kwanza ,la pili na la tatu pamoja na wale wa mahitaji maalum,sasa hawa bado ni watoto wadogo sana ambayo wanahitaji uangalizi wa kutosha wanapovuka barabara hasa ikizingatiwa hii ni barabara kubwa ,kwa hiyo nalishukuru sana jeshi la polisi mkoa wa  Dodoma kwa kuona chagamoto hii na kuifanyia kazi.

Kwa upande wake Ester Ngailo anaiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kuendelea kuipatia chagnamoto hiyo ufumbuzi hususan katika shule ambazo zinapitiwa na barabara kubwa katika mkoa kwa lengo la kuwanusuru watoto na ajali zinazoweza kuwasababishia ulemavu wa kudumu au vifo.

Programu Jumuishi ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali’ ya Mtoto (PJT-MMMAM) imeelekeza mambo matano ya kuzingatia katika Malezi ya watoto ili waweze kufikia ukuaji timilifu kuwa ni pamoja na Afya Bora,Lishe ya kutosha,Malezi yenye mwitikio,ujifunzajibwa awali pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto ili aweze kukua na kufikia utimilifu wake kwa ajili ya kuwa na Taifa lenye watu wenye tija.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Hazina Samwel Mziba anasema , akiwa kama kiongozi wa Kta hiyo ameshuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zimehusisha watoto wa shule hiyo huku akisema anaendeea kulifanyia kazi suala la mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule hiyo ili zoezi la kusimamisha magari na kuwavusha wenzao liwe enedelevu.

 Akizungumza na mtandao huu ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Theopista Malya anasema Jeshi hilo linapenda kila maeneo ya shule zilizo barabarani kuwe watoto wanaovusha wenzao kwa usaidizi wa askari lakini kwa sababu maeneo hayo ni mengi na askari ni wachache,Jeshi Hilo litaendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi ili waweze kuvuka barabara katika hali ya usalama huku akimwagiza Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Dodoma kufuatilia ili wanafunzi wa shule hiyo ya Mlezi waweze kufanya azi hiyo kwa usahihi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ajali za barabarani ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto  na vijana wenye umri wa miaka  mitano hadi 29 ambapo nchini Tanzania takwimu zilizotolewa na kikosi cha usalama barabarani zinaonesha kuanzia mwaka 2010 hadi Oktoba 2020 zimetokea ajali za barabarani 142,140 na kusababisha vifo vya watu 32,899 wakiwemo watoto.