Na Joyce Kasiki ,Timesmahira online,Dodoma
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)limeanza kuhudumia wateja wake kidijitali kupitia mfumonwake wa NIKONECT ikiwa ni agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka mashirika ya umma yajikite katika matumizi ya mifumo ya kidijitali.
Akizungumza na waandiahi wa habari kwenye maoneaho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma
, Afisa huduma kwa wateja wa TANESCO) Fatuma Mohamed amesema mfumo huo wa NIKONECT unatoa huduma kuanzia maunganisho ya umeme huku akisema pia wamepanua wigo katika matumizi ya TEHAMA kwa upande wa kutoa taarifa kwa jamii.
“Kupitia mfumo wetu wa kidijitali wa NIKONECT , mteja sio lazima afike ofisini ili kupata huduma ya kuunganishiwa umeme, isipokuwa mahali popote mteja ,awe na simu au hata simu ya kitochi , anaweza kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme na akapata huduma hiyo.”amesema Fatuma
Aidha amesema katika utoaji wa taarifa kwa kutumia TEHAMA,wigo umepanuka zaidi ambapo kwa kutumia mfumo wa JISOT , mteja anaweza akatoa taarifa kwa njia ya simu yake ya mkononi.
“Kwa kutumia JISOT taarifa hiyo inatumwa kupitia namba ya kutolea taarifa kwenye kituo cha miito ya simu Tanzania TANESCO ambayo ni 0748550000 ambayo pia inatumika kwa mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwa kutuma ujumbe Hi au Hello.”amesisitiza Fatuma
Aidha amesema faida ya huduma hizo ni kuokoa muda wa mteja kusafiri pamoja na usumbufu wa kutafuta ofisi ili kujipatia huduma lakini pia TANESCO wameweza kupata taarifa kwa haraka kiganjani na urahisi wa kuhudumia mteja kwa uharaka.
Vile vile amesema Shirika hilo linatumia mitandao mbalimbali ya kijamii katika kuuhabarisha umma kidijitali kuhusu masuala ya umeme ikiwemo Whatsapp, Instagram na (X) Twitter zinazotoa huduma kwa wateja.
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania