Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Jimbo la Mbulu Mjini lina Vijiji 34 ambapo Vijiji 31 kati ya hivyo vimepata umeme.
Ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma ambapo amesema uwa kwa Vijiji vilivyosalia utekelezaji wa miradi unaendelea na kazi itakamilika tarehe 30 Juni 2024.
Ameongeza kuwa, Jimbo la Mbulu Mjini lina mitaa 58 ambapo mitaa 46 ina umeme na mitaa 12 ambayo imesalia itapatiwa umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme vitongojini ambao utaanza mwaka wa fedha 2024/2025.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake