November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ijue kesho yako yawakumbusha wanawake kuishi maisha asilia

Na Esther MachaTimesmajiraOnline,Mbeya

WANAWAKE Mkoani Mbeya wametakiwa kuyaishi maisha yao wenyewe badala ya kuishi kwaajili ya watu wengine na kujisahau wao jambo ambalo limekua likikwamisha ndoto za wasichana na wanawake wengi Kwa kufikiria wanaishi kwaajili ya familia zao pekee.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa taasisi ya Ijue kesho yako Kwa Kuioambania Leo Rehema Mwalupindi, katika hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo Mkoani Mbeya ambapo amesema, kumekua na dhana iliyo jengeka Kwa wasichana na wanawake kuishi Kwaajili ya familia na watoto, jambo ambalo hupelekea wengine kuacha shughuli za uzalishaji ili waishi kwa furaha na familia ili hali wao hawana furaha.

Mwalupindi amesema lengo la kuanzishwa taasisi hiyo ni kutoa elimu zaidi Kwa wasichana na wanawake, ili kuwajengea uwezo wa kujitambua na kujua thamani yao ili kupata nguvu ya kufikia malengo yao waliyojiwekea.

“Lengo la taasisi hii ni kutoa elimu kwa wanawake pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kujitambua katika majukumu yao ya kila siku na jamii kwa ujumla “amesema Mwalupindi.

Imani Homera ni miongoni mwa wanawake walio shiriki katika hafla hiyo amewaomba taasisi hiyo kuongeza nguvu zaidi katika kusaidia wasichana kupata elimu hiyo hasa maeneo ya vyuo na vyuo vikuu kutokana na Hali mbaya ya maadili maeneo hayo.

“Maeneo ya vyuo vikuu kwa mabinti elimu bado inahitajika sana hivyo niombe taasisi hii ijikite sana maeneo ya vyuo msaidie mabinti zetu mabadiliko hamna kabisa”amesema Iman Homera ambaye ni mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo baadhi ya watoa mada walieleza umuhimu wa mwanamke katika malezi ya watoto ili waweze kukua katika mabadiliko yaliyo mema hasa katika kipindi hichi cha mabadiliko ya tabia nchi.