Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
TAASISI ya Kumbilamoto Foundation imetoa bima ya afya kwa Watu 114 bure wa kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoa Dar es Salaam, kwa ajili ya kusaidia wananchi huduma za matibabu katika hospitali na vituo vya afya..
Uzinduzi huo wa kugawa Bima ya afya ulianzia Zahanati ya Vingunguti ulinzinduliwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde ambapo aliwapa kadi za Bima ya afya kaya 19 sawa na Wananchi 114 wa mitaa sita ya Vingunguti.
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said akiizungumza mara baada kuzindua ugawaji wa Bima ya Afya Bure kwa watu 114,alisema mtaji wa mwanadamu ni afya hivyo TAASISI ya Kumbilamoto Foundation imejali afya za wananchi wa Vingunguti ni jambo la kumshukuru Mwenyenzi Mungu kila wakati.
“MWENYEKITI SIDDE alisema kadi ya Bima ya afya ni muhimu unaweza ukaitumia kupimia matibabu mpaka ya shilingi 700,000 au milioni kwa ajii ya vipimo peke yake hivyo wananchi wana umuhimu wa kukata bima ya afya tunaishukuru taasisi ya Kumbilamoto Foundation kwa kujali wananchi wa kata ya Vingunguti alisema Sidde
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbilamoto Foundation Omary Kumbilamoto alisema Taasisi ya Kumbilamoto Foundation imeanzishwa mwaka 2021 na kusajiliwa kwake mwaka 2022 inatoa huduma za kijamii sehemu zote ikiwemo kuchimba visima na kusaidia makundi maalum wakiwemo Wazee Wajane na Vijana ili kuondoa changamoto zao
Mwenyekiti wa Kumbilamoto Foundation Omary Kumbilamoto, alisema miaka mitatu ya Dkt.Samia Suluhu Hassan nchi yetu imepata mambo makubwa ya maendeleo ambapo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura na Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo Kata ya Vingunguti na jimbo la Segerea kwa ujumla .
Katibu wa Taasisi ya Kumbilamoto Foundation Alex Buberwa alisema wananchi 114, wamepewa kadi bure zenye thamani ya shilingi millioni 2.8 alisema taasisi hiyo imejikita zaidi kusaidia jamii leo wametoa mitaa sita ya Vingunguti ikiwemo Mtakuja,Majengo Mtambani,Butiama,Miembeni na Kombo kwa lengo la wananchi wa maeneo hayo waweze kuzitumia kadi hizo katika huduma ya afya.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti ISACK MAKUNDI alisema kwa sasa Zahanati ya Vingunguti inatoa huduma masaa 24 baadhi ya huduma hizo Kinywa na Meno ,Tiba ya mionzi (Utrasound )Wodi ya Wazazi kwa ajili ya kuzalisha kiliniki ya Baba Mama na Mtoto,TB na Ukoma ,Upasuaji mdogo ,matibabu ya wagonjwa wa nje .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa