November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Nchimbi:Kufanyika kwa maandamo kunasaidia kutangaza uwepo wa demokrasia nchini

Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline, Kilimanjaro

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema Chama cha CCM hakina sababu ya kukasirishwa na maandamano yanayofanywa na baadhi ya Vyama Pinzani ikiwemo CHADEMA, kwani kufanyika kwa maandano hayo kunaisaidia Serikali kutangaza uwepo wa Demokrasia nchini.

Nchimbi ameyasema hayo leo Juni 4, 2024 wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika Mkoa huo, ambapo amesema kuandamana kwa vyama pinzani ni kujidhihirisha uwepo wa Demokrasia.

Huku akisema, Suala la Demokrasia Rais amedhamiria kusimamia misingi ya Demokrasia kutoka ndani na nje ya chama ili  watanzania wapate uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

“Tundu Lisu na wakina Mbowe wanatusaidia hivyo tunawashukuru sana kwa kufanya kazi ya CCM na na kuonesha Serikali inajari suala la Demokrasia na kama wangeitaji kulipwa kweli ningewalipa kwa kazi nzuri wanayofanya hivyo hatuna sababu ya kuchukia,”amesema Nchimbi.

Aidha amesema, CCM kwa asilimia kubwa imeendelea kutimiza azma yake huku akidai kuwa, tangu kupata uhuru wa nchi hakuna kipind ambacho miradi ya maendeleo imetekelezwa kwa wingi kama inayotekelezwa.

Pia, amewata wananchi wa Jimbo la Hai kuwa wavumilivu na kusema kuwa changamoto zinazowakabili zitatatuliwa, huku akitaja Wizara ya Elimu na TAMISEMI kufanya  tathimini katika shule zote za zamani na kuzifanyia maboresho, huku akiahidi changamoto ya uwepo wa ubovu wa miundombinu ya barabara CCM kuzifanyia kazi.

“Tangu tupate uhuru hakuna awamu ambayo imewahi kuleta kwa wingi kama awamu hii ya sasa na hiyo yote ni kwa sababu ya Rais wetu ambaye mwanamke mwenye huruma, msikivu na mwenye upendo kwa watu wake, ametuletea shule, zahanati, vituo vya afya, vifaa tiba vingi na miradi ya maendeleo ya miundombinu ya barabara”, amesema Nchimbi

Naye Katibu wa NEC, Itifaki, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), hakijawahi kuiba kura na hakina mpango huo chaguzi zote chama hicho kimeshinda kihalali.

Makalla amewatoa hofu wananchi wa Jimbo la Hai kufuatia kauli za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama pinzani kuhusu CCM na kudai kuwa Chama cha CCM hakijawahi na hakipotayari kuiba kura katika chaguzi zote.

Amesema, Chama cha CCM kipo imara hivyo ni wajibu wa wananchi kuchagua viongozi sahihi kutoka CCM ili waendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.

“Msiwasikilize wale, kuna baadhi ya viongozi wanapotosha mfano kuna kiongozi mmoja wa Chama pinzani nimesikia akihutubia katika mkutano leo na katika sehemu ya maneno yake amesikika akiwaambia wananchi kuwa tusikubali CCM ishinde katika vijiji na mgombea wetu kukatwa na kama akikatwa basi yule aliye hapa tutashughulika naye”, amemnukuu Makalla huku akisema kauli hizo ni za mtu anaye ‘tapatapa’.

Amesema, CCM Haina mpango wa kufikilia masuala hayo na badala yake inafikiria kuhusu maendeleo ya wananchi na ziara zinazofanywa na chama hicho ni katika kuhakikisha inawafikia wananchi wake na kutatua kero zao, huku akiwasisitiza wananchi kutofanya makosa katika chaguzi zijazo na kuchagua wagombea kutoka CCM.

Makalla amesema kasi ya maendeleo kwa sasa ni kubwa hususani katika Jimbo la Hai tofauti na iliyokuwa awali na kusema kubwa ufanisi huo wa Chama unadhihirishwa na Wabunge wa CCM kwa wananchi wao.

” Niwaombe ndugu zangu tusifanye makosa, wakati ule tulifanya makosa tukakosa Jimbo la Hai, Siha, Moshi Mjini, Same Kusini nk, lakini Mwaka 2020 tulifuta makosa na CCM inachukua majimbo yote hivyo nategemea hata Sasa itakuwa hivyo hivyo majimbo yote kwenda kwa wagombea wa CCM”,amesisitiza Makalla.

Makalla amesisitiza kuwa, wananchi hawapaswi kupewa kauli za vitisho na kuraghaiwa na baadhi ya viongozi wa vyama pinzani na badala yake wananchi waache wawe na uhuru na haki ya kukupigia kura chama wananchi ridhishwa nacho.

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla, amesema ni vyema wananchi wakaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususani katika kumuombea pindi anapokuwa nje ya nchi kwa safari hizo zipo kwa ajili ya manufaa ya wananchi kwa ujumla.