Na AgnesAlcardo,
TimesmajiraOnline,Kilimanjaro
KATIBU wa NEC, Itifaki, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM),hakijawahi kuiba kura na hakina mpango huo chaguzi zote chama hicho kimeshinda kihalali.
Makalla amesema hayo leo,Juni 4,2024 wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ya siku mbili katika Mkoa huo, ambapo amesema Chama hicho katika chaguzi zijazo kimejipanga kushinda kwa kishindo.
Makalla amewatoa hofu wananchi wa Jimbo hilo kufuatia kauli za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama pinzani kuhusu CCM na kudai kuwa Chama cha CCM hakijawahi na hakipotayari kuiba kura katika chaguzi zote.
Amesema,CCM ipo imara hivyo ni wajibu wa wananchi kuchagua viongozi sahihi kutoka CCM ili waendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.
“Msiwasikilize wale, kuna baadhi ya viongozi wanapotosha mfano kuna kiongozi mmoja wa Chama pinzani nimesikia akihutubia katika mkutano leo na katika sehemu ya maneno yake amesikika akiwaambia wananchi kuwa tusikubali CCM ishinde katika vijiji na mgombea wetu kukatwa na kama akikatwa basi yule aliye hapa tutashughulika naye,”amemnukuu Makalla huku akisema kauli hizo ni za mtu anaye ‘tapatapa’.
Amesema, CCM haina mpango wa kufikiria masuala hayo na badala yake inafikiria kuhusu maendeleo ya wananchi na ziara zinazofanywa na chama hicho ni katika kuhakikisha inawafikia wananchi wake na kutatua kero zao, huku akiwasisitiza wananchi kutofanya makosa katika chaguzi zijazo na kuchagua wagombea kutoka CCM.
Makalla amesema kasi ya maendeleo kwa sasa ni kubwa hususani katika Jimbo la Hai tofauti na iliyokuwa awali na kusema kubwa ufanisi huo wa Chama unadhihirishwa na Wabunge wa CCM kwa wananchi wao.
“Niwaombe ndugu zangu tusifanye makosa, wakati ule tulifanya makosa tukakosa Jimbo la Hai, Siha, Moshi Mjini, Same Kusini nk, lakini Mwaka 2020 tulifuta makosa na CCM inachukua majimbo yote hivyo nategemea hata Sasa itakuwa hivyo hivyo majimbo yote kwenda kwa wagombea wa CCM,”amesisitiza Makalla.
Makalla amesisitiza kuwa, wananchi hawapaswi kupewa kauli za vitisho na kuraghaiwa na baadhi ya viongozi wa vyama pinzani na badala yake wananchi waache wawe na uhuru na haki ya kukupigia kura chama wananchi ridhishwa nacho.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi