Na Joyce Kasiki Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Lindi Tekla Ungele ameiomba Wizara ya Maliasli na Utalii kutumia Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI),kuendelea kufanya utafiti ili waweze kupata suluhisho la kudumu kwa wanyama tembo na ndovu kwa kuwa wamekuwa wakiingia katika makazi ya wananchi na kufanya uharibifu.
Amesema,wanyama hao wamekuwa wakiharibu mazao,kujeruhi na wakati mwingine kuua wananchi na hivyo kusababisha taharuki miongoni mwa wananchi.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapi amesema lazima jitihada kifanyike za kuhakikisha wananchi wamekuwa salama.
Ungele amesema,hatua hiyo ya wanyama hao waharibifu kuingia katika makazi ya watu,imekuwa ikisababisha jofu miongoni mwa wananchi na hivyo kusababisha watoto kushindwa kwenda shule lakini pia wananchi kushindwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.
Akizungumza kuhusu kifuta machozi ,Mbunge huyo amesema ,katika eneo hilo bado Wizara haifanyi vizuri hasa katika mkoa wa Lindi .
“Mfano katika Wilaya ya Nachingwea fidia zimelipwa mwisho Disemba 2022 tu,kwa hiyo utaona hali ya ulipaji fidia jinsi inavyosuasua.”amesema Ungele na kuongeza kuwa
“Tangu hiyo 2022 , hakuna kifuta jasho ambacho kimelipwa kwa wananchi hadi leo,hii ni hatari na kazi kubwa imefanywa na Wizara hiyo kupeleka helkopta kuwasaka tembo kuwapeleka kwenye mbuga.”ameongeza kuwa
“Jitihada kubwa zimefanyika Wizara ya Maliasli na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa kutengeneza bomu baridi ni jambo jema lakini bado ni suluhisho la muda tu,”
Ungele amesema,Serikali imetumia guarana kubwa kuwafukuza tembo hao kwenda kwenye mbuga lakini bado wanarud tena kwenye makazi ya watu.
“Yaan hawa wanyama wakifukuzwa mbuga moja wanahamia nyingine , mfano wamefukuzwa Nachingwea wataenda Liwale, Namtumbo hivyo watakuwa bado wanazunguka maeneo hayo hayo.”
Kutokana na hali hiyo ameiomba Serikali itafute suluhisho la kudumu ili wanyama hao wabaki katika maeneo yao siku zote.
“Lakini pia sisi wana-Lindi tunaomba kifuta machozi kitolewe kwa wakati, hali ni mbaya sio shwari kwa Mkoa wa Lindi na Wilaya zake,” amesisitiza Mbunge huyo
Ungele ametumia nafasi hiyo kumuomba Waziri na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii waende mkoani Lindi angalau kutoa neno kwa wananchi baada ya Bunge hili la bajeti kuahirishwa
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria