Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Manyara
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema hakuna mtu yoyote kutoka nje na ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) atakayeweza kuiongoza nchi ya Tanzania zaidi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Sumaye amesema hayo leo Mei 31, 2024 wakati akizungumzia na wananchi wa Katesh Wilaya ya Hanang, katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa ameongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano Kimataifa (Suki), Rabia Abdalla Humid, Ikiwa ni muendelezo wa ziara yao ya kutembelea Mikoa mitano na kukagua utekelezwaji wa Ilani ya CCM.
Sumaye amesema, kutokana na kazi kubwa ya kuendele kuleta maendeleo katika Mkoa wa Manyara, ni vyema wananchi wakaunga kwa pamoja kumuunga mkono Rais huyo kwa kumpa kura nyingi katika chaguzi zijazo ili chama hicho kiendelee kuwepo kwa ajili ya kupata maendeleo zaidi.
Pia, Sumaye amesema ana imani na sekretalieti ya CCM inayoongozwa na Balozi Dk. Nchimbi kwani inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha Chama kinaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani.
Aidha ameeleza kuwa, kazi kubwa ipo kwa watendaji wa Serikali na Chama ngazi za chini kuchapakazi kwa bidii ili kuwezesha upatikanaji wa ushindi kwa CCM.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda