October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndege ya Ryanair ikielekezwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Stansted mjini London kabla ya abiria kuanza kushuka.

Ndege ya Ryanair yalazimika kutua ghafla kufuatia tishio la bomu

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

NDEGE ya abiria ya Shirika la Ndege la Ryanair nchini Ireland iliyokuwa ikitoka mjini Krakow nchini Poland kuelekea mjini Dublin, Ireland imelazimika kutua ghafla baada ya ilani moja iliyokutwa chooni na kudai kuwa ndege hiyo ilikuwa na vilipuzi ndani yake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Msemaji wa Shirika la Ndege la Ryanair imeeleza kuwa, ndege imebadili mwelekeo hadi katika Uwanja wa Ndege wa Stansted mjini London ambapo maafisa wa polisi wa Essex wameikagua ndege hiyo.

Huku ndege mbili za kijeshi aina ya RAF Typhoon zikiiisindikiza ndege hiyo ya Boing 737-800 ambayo iliondoka Poland saa 5:35 jioni na ilitakiwa kutua Dublin Saa 7:35 usiku badala yake ikatua kwenye majira ya saa 12 jioni.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, ndege hiyo imefanikiwa kutua na kupelekwa eneo la mbali ambapo abiria walishuka.

Andy Kirby ni Afisa wa Polisi kutoka Essex amesema, “inaonekana kama ndege za kijeshi za Eurofighters zilikuwa zikizunguka juu ya anga ya Uwanja wa Ndege wa Stansted”.

Ryanair ni Shirika kubwa la Ndege nchini Ireland ambalo limesambaa kote barani Ulaya, linatoa huduma kupitia ndege 2500 kwenda kwenye vituo zaidi ya 200 katika nchi 40 duniani.