Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
Wabunifu kutoka Chuo Kikuu ikuu cha Dar-es-Salaam wamekuja na ubunifu wa kutengeneza vitambaa vya nguo kwa kutumia chupa za plastiki bila kuhusisha matumizi ya kemikali ambazo zinamadhara kwa binadamu.
Wabunifu hao wameonesha umuhimu wa mitaji kuendeleza bunifu zao ili ziweze kukua na kusaidia kukabiliana na changamoto za ajira nchini.
Moja ya bunifu walizozifanya wanafunzi kutoka katika chuo hicho ni pamoja na kuyeyusha chupa za plastiki na kwenda kutengenezea nguo ugunduzi huo unaonekana kuwavutia watu wengi.
Akizungumza na Timesmajira katika maonesho ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Popatlal,Wanafunzi wa chuo hicho akiwemo Daudi Nzunda amesema wanafanya ubunifu huo kwa kutumia mashine inayogeuza chupa hizo za plastiki kwa kuzisaga vipamde vidogo vidogo vinavyochomwa kwenye sehemu maalumu kwa kugandamizwa .
Kisha vinavyotengeneza nyuzi ndogo ndogo ambazo zinatengenezwa kuwa maalumu zinazoweza kutumika kushona vitu mbalimbali.
“Inasemekana kwamba zaidi ya tani milioni 350 za plastiki zinatengenezwa kila mwaka,pia zimesababisha uchafuzi mkubwa kwenye mitaro, baharini na kwenye vyanzo vya maji na maeneo mbalimbali kutokana na tatizo hili tumekuja na namna ambayo tunazigeuza hizi plastiki kuwa vitambaa ambavyo unaweza kushonea nguo, magauni, tisheti pamoja na vitu vingine vyote vikiwa na ‘material quality’ kabisa sawa na vitambaa vya polista,”amebainisha Nzunda na kuongeza kuwa ;
“Faida ya ubunifu huu kwanza ni nzuri kiuchumi sababu chupa za plastiki zinatosha kutengeneza kitambaa ambacho kinaweza kutengeneza tisheti lakini pia faida nyingine ni kwamba ‘project’ hii haihusishi matumizi ya kemikali ambazo zinamadhara kwa binadamu mbali na hilo faida nyingine itasaidia kuongeza na kuleta ajira kwa vijana kuanzia kwenye mzunguko mzima ukianzia kwa watu wanaookota chupa za plastiki mitaani kwa kusaidia kuongeza thamani ya plastiki zinazotupwa pamoja na watakaokuwa wanatumia mashine hizi kwajili ya kutengenezea vitambaa, “.
Mbali na hayo pia chuo hicho kimekuja na mradi wa kufundisha kiswahili hususani kwa wageni ambao kabla ya kuutengeneza walijaribu kuzunguka sehemu mbalimbali ambazo zinafundisha kiswahili kwa wageni ambapo waligundua kuwa bado kuna mbinu za zamani za ufundishaji wa lugha hiyo kwa watu hao ambao hufundisha kwa kuingia darasani.
Hivyo mara baada ya kufanya uchambuzi waliona upo umuhimu wa kuunda mfumo ambao mwanafunzi atakuwa anajifunza kiswahili hata wageni popote alipo duniani.
Mhadhiri kutoka chuo hicho Dkt. Kanijo Ponsiano amesema “Kiswahili sasa hivi ni biashara na watu wengi wamekuwa wakihitaji ndani ya Afrika na nje ya Afrika hivyo tumetengeneza mfumo ambao mwanafunzi anaweza kujifunza peke ake bila kuwa na mwalimu na tumepanga masomo yetu kwa namna ambayo ni ya kisasa kwa kutumia mfumo wa mawasiliano zaidi,”.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi