Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Kampuni ya mawasiliano Tigo, Imezindua App ya kisasa ya Tigopesa ‘Supper App’ ambayo imefanyiwa maboresho zaidi, ambayo itawafanya watumiaji wa huduma za kampuni hiyo kufanya miamala yao kwa urahisi zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Tigopesa, Angelica Pesha amesema App hiyo inaweza kufanya miamala ya fedha, miamala ya kawaida ya kufanya mawasiliano kwa kununua vifurushi na muda wa maongezi lakini pia kufanya malipo ya bidhaa
“Hii ni Appa ambayo inawezesha huduma zetu zote za Tigo kupatikana katika sehemu moja, App hii imekuja na vitu vingi vizuri na vya kisasa zaidi ikiwemo muonekano, Ina mionekano zaidi ya mitatu inategemea na wewe unapenda teknolojia kiasi gani”
“Muonekano wa kwanza ni ule ambao unaendana na app ya zamani, tusingependa wateja wetu waliozoea App ya zamani kupata shida, pia kuna muonekano ambao umeboreshwa zaidi lakini pia muonekano mwingine ni ule ambao watu wanapenda teknolojia ya kisasa”
Pesha amesema kwenye Supper App wamewezesha pia kutuma pesa kwa watu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
“Inawezekana unataka kutuma pesa kwa watu zaidi ya watatu, zamani ilibdi ufanye miamala mitatu, kwa sasa unaingia, unachagua mtu ambaye unataka kumtumia, unachagua ni shilingi ngapi unataka kutuma, ikiwa ni bei Moja kwa watu wote, au shilingi tofautitofauti tofauti, kitu ambacho hakikuwepo zamani”
Pia amesema katika App hiyo wameweka Min App ambayo inauwezo ya kuweka app nyingine ndani ya App Super App.
Kwa upande wa wafanyabiashara, Pesha amesema App hiyo itawarahisishia kuweza kufanya malipo ya mshahara na malipo yao yote tofautitofauti wanauwezo wa kufanya na kupokea malipo hayo kama mfanyabiashara wa lipa kwa simu.
Kadhalika, Pesha amesema kwa sasa wamewezesha App hiyo kuwepo kwenye simu zote hadi kwenye Smart kitochi
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi