Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga Leo, Mei 14, 2024, ameshiriki Mkutano wa Nishati Safi ya kupikia ambapo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mwenyekiti mwenza wa mkutano mkubwa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika yaani Summit of Clean Cooking in Africa unaofanyika Paris, Ufaransa.
Mkutano huu umewaleta pamoja wadau mbalimbali wa Nishati Safi ya Kupikia Duniani, kumuunga mkono, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameishikilia agenda hii kama kinara namba moja kwa nishati ya kupikia Afrika.
Rais, Dkt. Samia, ambaye ndiye kinara wa nishati safi ya kupikia Afrika na amefanikisha kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wadau wa kimtaifa katika Program hii muhimu yenye manufaa kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.
Katika mkutano huu wenyeviti wenza wengine ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dr. Akinwumi_adesina, Mkurugenzi Mkuu wa International Energy Agency (IEA) Fatih Birol na Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Støre.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa