November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hifadhi ya Taifa Katavi yaimarisha ulinzi na usalama kwa majangili

Na Mwandishi wetu,Katavi

MHIFADHI Mwandamizi wa Idara ya Himasheria na Ulinzi wa Kimkakati kutoka Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Benedict Mbuya amesema hifadhi hiyo imeendelea kuimarisha ulinzi na usalama wake katika kukabiliana na majangili wa wanyamapori.

Ameyasema hayo jana mkoani Katavi wakati akiongea na waandishi wa habari,Mhifadhi Mbuya amesema kutokana na ufanywaji wa doria za mara kwa mara katika hifadhi hizo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa majangili kutoingia na kufanya ujangili.

Amesema ujangili ambao wanakabiliana nao katika hifadhi hiyo ni pamoja na upasuaji wa mbao,uingizaji wa mifugo hifadhini ,uwindaji wa wanyama na vitoweo.

”Sisi kama hifadhi ya taifa ya Katavi tumeendelea kujipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika hifadhi yetu inaimarika na kukomesha hali ya ujangili katika hifadhi hiyo,”amesema.

Amesema katika kukabiliana na majangili hao wamekuwa wakishirikiana na wadau wengine pamoja na vyombo vya ulinzi kuhakikisha ujangili unaisha katika hfadhi hiyo.

Akizungumzia wananchi wanaoingiza mifugo katika hifadhi hiyo,Mhifadhi Mbuya amesema kwa wale watu wanaoingiza mifugo katika hifadhi hiyo kwa sasa ukamatwa na kufikishwa mahakama kisha ufunguliwa kesi ambapo mashauri yote ya mahakamani inakuwa inasubiria sheria kufata mkondo wake wa kupigwa faini.

Kwa upande wake,Afisa Uhifadhi daraja la pili ambaye ni Kaimu Mhifadhi Kitengo cha Mahusiano ya Jamii ,Meleji Mollel,amesema kwa mwaka huu mwezi Januari,askari wa doria walikama mbuzi 9,mwezi Februari Ng’ombe 73,Machi ng’ombea 166 huku mwezi wa Aprili hawakukamata mifugo yoyote ndani ya hifadhi hiyo.

Amesema hali ya ukamataji wa mifugo imepungua katika hifadhi hiyo kulingana na miaka ya nyuma kutokana na mahakama kutaifisha mifugo hiyo kwa kufanya mnada wa hadhara.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tukikamata ng’ombe wengi sanaa kipindi kama hiki ila kwa sasa tunaona hali inavyozidi kuimarika na watu hawaingizi tena mifugo yao hifadhini kwa kuhofia mifugo yao kupelekwa mahakamani kama sheria inavyosema,”amesema.