Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya.
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya imetenga zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya uboreshaji wa vyumba chakavu vya madarasa 300 katika shule za msingi zilizopo jijini humo .
Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za miradi ya maendeleo kilichofanyika Aprili 30,2024 Mkurugenzi Jiji la Mbeya ,John Nchimbi amesema tayari baadhi ya vyumba vya madarasa uboreshaji umeanza.
Amesema katika kutekeleza na kufikia malengo ya kukamilisha miradi ambayo inaelekezwa na Serikali ni vyema Madiwani kwenye maeneo husika ambako uboreshaji wa vyumba chakavu vya madarasa inafanyika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.
“Imani yangu kwa sasa wataalam wamekuwa wakiwashirikisha kwenye miradi inayokuja katika maeneo yenu na ndio maana imetekelezwa kwa wakati uliopangwa,”amesema.
Kwa upande wake Meya Jiji la Mbeya, DorMohamed Issa amesema kuwa halmashauri hiyo imepata hati safi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Issa amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano baina ya halmashauri,Madiwani na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye ni Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) ,Dkt, Tulia Ackson.
Issa ametaja miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la upasuaji ,wodi za wagonjwa wa upasuaji,jengo la dharura katika hosptali ya Wilaya ya Igawilo ambayo ilipandishwa hadhi baada ya kuwa kituo cha afya.
Hata hivyo amesema pia kuna ujenzi wa vituo vya afya na zahanati vinaendelea katika Kata zote za Jiji la Mbeya lengo ni kuboresha huduma kwa watanzania ifikapo 2025.
Ameongeza kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kama ujenzi wa matundu 300 katika shule za msingi na sekondari .
“Tayari kuna baadhi ya shule za msingi na sekondari uboreshaji umeanza ,mfano shule ya msingi Isanga tayari ipo kwenye uboreshaji wa vyumba chakavu vya madarasa”amesema.
Hata hivyo Meya huyo amesema wamepokea gari la wagonjwa kutoka kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambalo litakabidhiwa kituo cha afya Nzovwe jijini hapa ili kuboresha sekta ya afya na wananchi kujivunia matunda ya serikali yao
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili