Na Mwandishi wetu, timesmajira
MKURUGENZI wa Furaha Media, Furaha Dominick aliwataka vijana kupendana, kushirikiana, kusaidiana, kupeana fursa, kuneneana yaliyomema pamoja na kuishi katika mienendo ya kumpendeza Mungu.
Akitoa Salamu za pole leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mpiga picha na Mwandishi wa habari wa Millardayo na Ayo Tv, Noel Mwingila (Zuch Zuchero) aliyefariki dunia alfajiri ya Aprili 26, 2024 baada ya kupata ajali ya pikipiki maeneo ya Makonde – Mbezi, Dar es salaam , Mkuu huyo wa Wilaya alisema ni vema yale yote Zuch aliyoyafanya yanapaswa kuishi ndani yetu na kuyabeba.
“Ukimwangalia Zuch utagundua kuwa alikuwa mtu wa kujishusha sana, alikuwa na jina kubwa lakini hakuwahi kujikweza hata ukiangalia aliacha gari yake na kupanda bodaboda, hiyo yote ni kuonyesha kujishusha kwake,”amesema.
Amesema kifo chake kimesikitisha na kuumiza watu wengi lakini ni mipango ya Mungu ambayo haina makosa.” tunapaswa kushukuru kwa kila jambo, tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha ya Zuch hapa duniani,” amesema.
Amesema ni muhimu vijana wakapendana na kuneneana yaliyomema na kwamba linapotokea jambo lolote linalomgusa kijana mwingine wawe mstari wa mbele na kuungana na kusaidiana.
“Tumempoteza kijana aliyekuwa ashaanza kuaminika na hata katika ziara za Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuhudhuria hii inaonesha ni namna gani alivyokuwa anafanya kazi kwa kuaminika,”amesema na kuongeza
“Zuch amekuwa kijana wa kuigwa kwa namna alivyoishi na watu vizuri na kusaidia wengine hivyo Taifa limepoteza nguvu kazi na litamkumbuka daima kwa jinsi alivyokuwa kijana shupavu, mpambanaji na asiyebagua watu,”amesema
Zuch alikua ni mmoja kati ya wapigapicha mahili kwenye tasnia ya habari na matukio.
More Stories
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda
Ukosefu wa maji wasababisha wanafunzi kujisaidia vichakani