Taarifa zamfikia akiwa safarini kuelekea Dodoma katika Mkutano Mkuu wa CCM
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
MAMA mzazi wa mfanyabiashara maarufu visiwani Zanzibar na Mwakilikishi wa Jimbo la Uzini aliyemaliza muda kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, Kulthum Hassanali Mohamedali (83) amefariki.
Kifo cha Kulthum Hassanali Mohamedali kilichotokea jana (Julai 10, 2020) kimethibitishwa na Raza alipozungumza na www.timesmajira kwa njia ya simu leo. Mazishi ya Kulthum yamefanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
Raza amesema jana alikuwa na mama yake jijini Dar es Salaam na kuagana naye akiwa mzima wa afya na kupanda ndege kuelekea jijini Dodoma, lakini alipokuwa angani alikuwa akitafutwa, lakini hakupatikana kwa sababu simu yake alikuwa ameizima.
Amesema baada kutua Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kuwasha zimu ndipo alibaini kwamba alikuwa anatafutwa na ndugu zake wanaoishi na mama yake jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Raza alipowasiliana nao muda ule ndipo alipopewa taarifa za kifo cha mama yake. “Ni msiba wa ghafla sana, kwani niliachana na mama yangu akiwa mzima na nilizongumza naye vizuri,”amesema Raza kwa masikitiko.
Raza amesema mama yake, Kulthum Hassanali Mohamedali alizaliwa Januari 7, mwaka 1937 na kubahatika kupata watoto wanne ambao mbali na yeye, wengine ni Fatma Mohsin Hassanali, Mohamedraza Hassan na Ibrahim Hassanali.
Marehemu ameacha wajukuu 12 na vitukuu wanne. Mungu ailaze mahali pema peponi.
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania