Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma ya Zimbabwe (PRAZ) imeingia nchini kupata uzoefu wa uendeshaji wa michakato ya Ununuzi wa umma kupitia Mamlaka ya Udhibiti eats Umma hapa nchini (PPRA).
Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Dodoma Afisa Mtendaji Mkuu wa PRAZ Bw. Clever Ruswa amesema kuwa licha ya ziara hiyo kuwa ya muda mfupi lakini itatosha kujifunza na kubadilishana uzoefu wa uendeshaji wa masuala ya Ununuzi wa Umma baina ya Zimbabwe na Tanzania.
Bw. Ruswa amesema kuwa kilichowavutia zaidi Nchini Tanzania ni mafanikio ya ujenzi wa mfumo wa ununuzi kielektroniki uliojengwa na wataalamu wazawa suala ambalo kwake ameliita kuwa ni uthubutu wa hali ya juu kwa Serikali ya Tanzania.
“ Kitu kikubwa ambacho Zimbabwe wanaona kuwa ni mafanikio kwa Serikali ya Tanzania ni kuwa na mfumo wa kielektoniki wa ununuzi amabao umejengwa na wataalamu wa kitanzania, hakika huu ni uthubutu wa hali ya juu. Alisema Bw. Ruswa.
Sambamba na hilo Bw. Ruswa ameweka wazi matarajio ya ziara yao hiyo kuwa hawategemei kutoka patupu badala yake watapata mambo mengi mazuri ya kujifunza kupitia PPRA ikiwa ni pamoja na namna ya kupata ufanisi katika ununuzi wa Umma kupitia mfumo wa NeST ambao unatumika na PPRA katika kuendesha michakato ya utoaji wa zabuni za umma.
Mfumo wa NeST umeanza kutumika rasmi mwezi Julai 2023 ambapo mpaka leo Aprili 14, 2024 Jumla ya mikataba ya zabuni 12320 yenye thamani ya TSH Trilioni 3.35 tayari imeshatolewa.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa