Na Penina Malundo, timesmajira
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni,amewatembelea na kuwajulia hali askari wawili wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila jijini Dar es Salaam wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupata kujeruhiwa wakati wakiwa katika harakati za kuokoa majeruhi walipata ajali eneo la Mlandizi mkoani Pwani.
Askari hao walipata majeraha katika zoezi la ukoaji wa ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria na gari yay mafuta iliyotokea Machi 28 mwaka huu saa 10:15 alfajiri maeneo ya Ruvu mkoani Pwani .Askari waliojuliwa hali na Waziri Masauni ni pamoja na 3463 Koplo Hamisi Kungwi ambaye yupo chumba cha wagonjwa mahututi na 3384 Koplp Elias Bwire ambaye yupo wifi ya wagonjwa wa kawaida.
Akizungumza baada ya kuwajulia hali wagonjwa hao,Mhandisi Masauni amesema amefurahishwa na namna wataalam wa afya wa hospitali hiyo walivyowahudumia wagonjwa hao kwa weledi na kujituma ambapo kwa sasa hali ya wagonjwa hao inaendelea vizuri.
“Nimefurahishwa na hali ya utoaji huduma katika hospitali ya Mloganzila kwani ina mazigira mazuri na usafi wa hali ya juu tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini Raii Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji alioufanya katika Sekta ya Afya” amesema Mhandisi. Masauni
Amesema serikali inaendelea kuliangalia eneo la uwekeza katika mafunzo ili kuwasaidia askari wanapotekeleza majukumu yao wawe na uelewa mkubwa zaidi.”Niliyòyasikia na kuyaona ni zaidi ya matarajio, nimekuja nakujionea mwenyewe jinsi ambavyo afya za askari hawa zinavyoendelea kuimarika, kiukweli huduma na mazingira ya hospitali ni mazuri sana, tunazidi kuwaombea ili afya zao ziendelee kuwa nzuri na hatimaye warudi nyumbani kuungana na familia zao,” amesema Waziri Masauni
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila, Dk. Julieth Magandi amesema askari haw wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo.”Sisi madaktari tunatibu ila Mwenyezi Mungu anaponya hivyo tunaendelea kuwaombea ili waweze kupata nafuu ya haraka na afya njema wapone ili watoke hospitali waendelee na majukumu yao ya kawaida,”amesema na kuongeza
“Tunamshukuru Rais kwa namna ambavyo Serikali yake imewekeza kwa lengo la kuhakikisha huduma zinatolewa,sisi tuna ahidi tutaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kama serikali inavyotutaka tufanye,” amesema Dk. Magandi
Kwa upande wa askari ambaye amèlazwa hospitali hapo, Koplo Bwire amesema anamshukuru Waziri na serikali kwa ujumla kwa kuweza kuwajulia hali na kuwapa mkono wa pole.”Hii ni ajali kama zilivyoajali nyingine, ni kweli tumepata ajali tukiwa kazini lakini tunashukuru kwa namna ambavyo tumepata huduma, nakushukuru sana Waziri wa kufika hospitali hapa na kutujulia hali Mungu akubariki sana,” amesema Bwire
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu