November 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ilala kujenga uwanja wa mpira wa kisaa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema mikakati ya wilaya ya Ilala kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira ndani ya wilaya Ilala kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alisema hayo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu Bonnah cup Jimbo la Segerea 2024 .

“Mikakati ya wilaya yetu ya Ilala kujenga uwanja wa nyasi wa kisasa ndani ya wilaya yetu ya Ilala nia tunayo na uwezo tunao sababu Halmashauri yetu ya jiji kwa sasa inajusanya mapato makubwa hivyo nitawashauri madiwani wa Halmashauri waweze kutenga pesa za michezo “alisema Mpogolo.

Mpogolo alisema dhamira ya mashindano ya Bonah Cup jimbo la Segerea kujenga umoja na mshikamano hivyo mara baada kumalizika kwa uwanja wa kisasa wa nyasi utatumika katika shughuli za michezo kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo katika wilaya ya Ilala.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kwa kuunganisha umoja na mshikamano timu zote 61 kutoka ndani ya Jimbo la Segerea ambapo ameweza kuunganisha makundi ya Bodaboda, Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, na Chama cha Mapinduzi CCM na Wenyeviti wa Serikali za mitaa yote ya Jimbo la Segerea.

Alisema Halmashauri hiyo imetenga shilingi Bilioni 8 kwa ajili ya mikopo hivyo shilingi Bilioni 2 hawawezi kukosa kwa ajili ya Bajeti ya Michezo.

Katika hatua nyingine aliwataka Watendaji wa Kata kwenda kuwajenga vijana wawe wana zungumzia maadili pamoja na Polisi Kata wawe wana zungumzia usalama na Ulinzi na sekta ya uchumi katika michezo..