Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
MBUNGE wa Jimbo la Nkasi Kusini mkoani Rukwa Vicent Mbogo amesherekea sikukuu ya Pasaka kwa kula pamoja na Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Kata ya Chala pamoja na Wananchi na kuutumia muda huo kukusanya mawazo kutoka kwao ambayo atakwenda kuyapeleka Bungeni.
Akizungumza na viongozi hao Mbogo ameeleza kuwa kuna wakati ni ngumu kwa watu kuweza kukutana na Mbunge na kumueleza mambo ya msingi hivyo kwa kuona hilo ameamua kuitumia sikukuu ya Pasaka ili kuwarahishia Wananchi kuzungumza mambo ambayo wanafikiri yanaweza kuzungumzwa na kupewa kipaumbele na mwakilishi wao katika utekelezaji.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chala Johakimu Mwakampya amewataka Wajumbe wa mkutano huo kuitumia nafasi hiyo kueleza mambo ya msingi ili Mbunge wao aweze kuyachukua na kwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya maendeleo yao.
Baadhi ya Wananchi akiwemo Emmanuel Masunga,wamemueleza Mbunge huyo awe macho kwa watendaji wanaotekeleza miradi hiyo kwa kuwafuatilia ili itekelezwa sawa na thamani husika ya fedha zilizotolewa na serikali.
Diwani wa Kata ya Chala Michael Mwanalinze amempongeza Mbogo kwa namna anavyowawakilisha bungeni na jimbo hilo kuweza kuwa na miradi mingi ya maendeleo na kuwa na wao kama viongozi wa chini yake wanahakikisha kuwa wanamsaidia katika kusimamia miradi hiyo ya maendeleo
Pia ametumia nafasi hiyo kumueleza Mbunge huyo kuwa asiwe na wasiwasi na asipende kupokea maneno kutoka kwa watu yenye lengo la kuwachonganisha kwani huu ni wakati wa kuwa pamoja na kushikamana ili kile walichowaahidi wananchi kiweze kutekelezeka na wakakiona.
Awali Katibu wa Kata hiyo Edwini Mwanakulya amemtaka Mbunge kuendelea kuwakutanisha Wananchi na kuweza kuzungumza mambo yao kwa uwazi badala ya kila mtu kumtafuta kwa wakati wake kitu ambacho kinaleta usumbufu.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â