November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia apongezwa kugusa jamii na wenye uhitaji

Na Esther Macha Timesmajira Online, Mbeya

MJUMBE wa Baraza kuu la UVCCM Taifa kutoka mkoa wa Mbeya ,Timida Fyandomo amempongeza Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson kutokana na kutambua jitihada kubwa anazofanya za kusaidia jamii na watu wenye uhitaji.

Dkt.Tulia ambaye pia Spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani (IPU)pamoja na pongezi hizo Fyandomo amesema Dkt Tulia ni kiongozi wa mfano ambaye vijana wa mkoa wa Mbeya wanamuunga mkono katika utendaji wake.

Fyandomo amesema hayo leo wakati alipotembelea ujenzi wa nyumba inayojengwa na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Tulia ambapo Mama mjane aliyekuwa akiishi na watoto wake sita(6) kwenye nyumba iliyojengwa kwa maturubai iliyopo mtaa Itanji kata ya Iganjo Jijini Mbeya.

“Licha ya majukumu yake inabidi awatekelezee wananchi wa Mbeya Mjini lakini ameweza kugusa makundi mbalimbali vile vile ameweza kumgusa mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake ,ni juzi tu tumeona alikuwa anagawa bima za afya kwa zaidi ya wananchi 6000 ,lakini bado yupo kwenye ujenzi na hii ni nyumba ya tisa anayojenga na nategemea kabisa ana mpango wa kujenga zaidi ya hizo na hizi nyumba za wahitaji hajajenga tu kwa wilaya ya Mbeya mjini ,Mimi natokea wilaya ya Rungwe amejenga pia ambako sio jimbo lake kwa hiyo mimi nampongeza sana Dkt.Tulia “amesema Fyandomo.

Hata hivyo amesema kuwa anampongeza Dkt.Tulia kwasababu anaishi na kutekeleza dhana ya Mh Rais Samia ya kuleta maendeleo kwa jamii kwa vitendo leo amejenga nyumba hii kesho kutwa atajenga nyingine na nyingine na kuwa kama kiongozi wa vijana na Binti ambaye anajifunza mengi kutoka kwa Dkt.Tulia kwa mambo makubwa ambayo amekuwa akifanya katika uongozi wake .

“Mimi nimekuja kuangalia ujenzi huu unaofanywa na Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Dkt.Tulia ni vitu gani naweza kuunga juhudi kwa kazi kubwa inayofanywa na Dkt.Tulia ili na mimi niwexe kuchangia hivyo siku ya kukabidhi nyumba hiyo nitatoka Godoro na jiko.la gesi na pamoja na vyombo nimekuja hapa kujionea na kumpongeza Dkt.Tulia na kutoa ahadi kwa mama yangu “amesema Fyandomo.

Kwa upande wake Ofisa habari na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust,Joshua Mwakanolo amesema kuwa nyumba ambazo zimejengwa mpaka Sasa ni tisa na kwamba ndani ya Jiji la Mbeya itakuwa nyumba ya Saba hivyo kwa mkoa mzima wa Mbeya itakuwa nyumba ya tisa.

“Tunamshukuru sana mjumbe wa baraza ku umoja wa vijana kwa kumpa tabasamu na kutoa ahadi ya godoro na kusema wakati ukifika mjumbe huyo atakabidhi vitu vingine kwa hiyo tunashukuru kwa moyo wake wa upendo kwani tunao viongozi wengi lakini kaguswa na hili ,sisi kama vijana tunasema tutamuunga mkono zaidi kwa kuunga mkono jitihada za Dkt.Tulia ambaye ni Mbunge wa jimbo la mbeya na Spika wa bunge na Rais wa umoja wa mabunge duniani”amesema Mwakanolo.

Akitoa shukrani zake kwa mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa Mama huyo mjane mwenye watoto sita ,Singwava Jackson amesema kuwa alinunua uwanja na kujenga nyumba ya maturubai baada ya kufukuzwa na shemeji yake nyumbani alikokuwa akiishi na watoto wake .

Amemshukuru Dkt.Tulia kwa kumuona na kumsaidia na kuomba Mwenyezi MUNGU ampe nafasi nyingine kubwa ya uongozi.