November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaimu Ofisa Fedha kutoka Benki ya NMB Benedicto Baragomwa (wapili Kulia) akimkabidhi madawati Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu kwaajili ya kusaidia shule Saba za sekondari zilizopo jijini Tanga katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari pongwe Leo. Picha na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga.

NMB yatoa msaada wa mil.36 kwa shule sekondari Tanga

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

BENKI ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya sh.Mil 36 kwa shule saba za sekondari za Jiji la Tanga kwa kuzipatia madawati 250 na mabati 352 kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto za kielimu nchini.

Akikabidhi msaada huo katika shule ya sekondari ya Pongwe kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummi Mwalimu,Kaimu Afisa Mkuu wa fedha Benedicto Baragomwa alisema wamekuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Alisema kwa upande wa sekta ya elimu kipaumbele wamekiweka kwenye madawati, vifaa vya kuezekea huku kwenye afya tukitoa vifaa tiba kama vitanda vya kujifungulia wakina mama na vitanda vya wagonjwa na magodoro yake na kusaidia majanga yanayoipata nchi.

Alisema kuwa kutokana na kutambua juhudi kubwa za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano hivyo wameona ipo haja ya kuhakikisha inatoa sehemu ya faida yake katika kuchangia juhudi hizo.

Kaimu Ofisa Fedha kutoka Benki ya NMB Benedicto Baragomwa (wapili kushoto) akimkabidhi mabati Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwaajili ya kusaidia shule saba za sekondari za Jiji la Tanga katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari pongwe Leo. Picha na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga.

“Tumekuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii hivyo changamoto katika sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vyetu Kama benki kwani tumekuwa tukishiriki katika kusaidia jamii na tumekuwa tukisaidia pia katika sekta ya afya “alisema Baragomwa.

Alisema kuwa katika kipindi Cha miaka minne benki hiyo imekwisha changia zaidi ya shilingi Bil nne kusaidia jamii katika ununuzi wa vifaa tiba330 kwa hospitali na vituo vya Afya,zaidi yamadawati 31,150 pamoja na kompyuta1,150 nchi nzima.

“Mwaka huu wa 2020 NMB imetenga zaidi ya sh Bilioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu”alisema Baragomwa.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa elimu bure imeweza kusaidia watoto wengi wa kike kupata fursa ya elimu tofauti na hapo awali ilivyokuwa.

Hata hivyo alisema kuwa jitihada za serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia ni katika kuhakikisha wanaongeza ufaulu wa wanafunzi.

“Tunawashukuru NMB kwa kuweza kutuunga mkono katika jitihada za kumaliza changamoto za kielimu katika Jiji la Tanga hususani katika upande wa uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati”alisema Waziri Ummy.

Benki hiyo imesema itaendelea kuunga mkono serikali katika kusaidia changamoto mbalimbali kwa jamii ambapo imetoa msaada wa madawati 250 pamoja na mabati 352 kwashule za sekondari ya Kirare, Japan, Chongoleani, Nguvumali,Pongwe na Galanos.