January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Leah aunga mkono Juhudi za Rais Samia, agawa mitungi ya gesi

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

DIWANI wa kata ya Kinyerezi Leah Mgitu ameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kugawa mitungi ya Gesi kwa wafanyabishara wa Kinyerezi pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi.

Diwani Leah mgitu aligawa mitungi hiyo ya gesi jana katika kampeni yake endelevu ya kuunga mkono juhudi za Serikali wananchi waache kutumia nishati ya mkaa wasiaribu vyanzo vya maji na kusababisha nchi kuwa jangwa .

“LEO wajasiriamali wa kata yangu na viongozi wa chama nimewapatia mitungi ya gesi ili kumuunga mkono Rais wananchi waache kutumia nishati ya mkaa ,waanze kutumia gesi na nishati mbadala “alisema Leah.

Diwani Leah mgitu alisema Kampeni hiyo ni endelevu kuaiikisha wananchi wa Kata ya Kinyerezi watumie nishati mbadala na majiko ya gesi ya kisasa.

Aidha alisema Dhumuni lake lingine la kugawa mitungi hiyo ya gesi ni kutunza mazingira bora ya kata ya Kinyerezi ambayo yataenda sambamba na kampeni ya kupanda miti ya matunda na vivuli ili kuakikisha Kinyerezi inakuwa ya kijani

Alisema kampeni hiyo ya kupanda miti inatarajia kuanza Mwezi April mwaka huu ambapo atashirikiana na Wananchi wa kata hiyo kila kaya ipande miti mitano ya matunda na vivuli.