Tigo yachaguliwa kuwania Tuzo ya ITU WSIS 2024 Kupitia mradi wa UCSAF (Mfuko wa mawasiliano kwa wote)-Zanzibar, Mradi wa Tigo wa Mawasiliano ya Vijijini huko Zanzibar, kwa ushirikiano na UCSAF umependekezwa kuwania Tuzo za ITU WSIS 2024.
Mradi huo umechaguliwa baada ya kufanikiwa kushughulikia changamoto za mawasiliano kwa kutambua maeneo 42 katika kata 38 kwa kupitia Serikali. Tigo Zantel, kama mtoa huduma mmoja wa pekee, walikamilisha mradi huo kwa muda wa takriban chini ya mwaka mmoja ambapo watu 211,601 wamenufaika na mradi huu.
Nyote mpigie kura mradi wetu ili kushinda tuzo hii ya kimataifa yenye heshima kwa kufuata hatua rahisi zifuatazo:
Hatua 1: Bonyeza kwenye URL ifuatayo: https://www.itu.int/net4/wsis/stocktaking/Prizes/2024 Hatua 2: Bonyeza kitufe cha Piga Kura na tengeneza akaunti mpya. Hatua 3: Kwenye menyu kuu, Chagua Kura Hatua 4: Chini ya WSIS 2024, Chagua AL C2. Miundombinu ya Habari na Mawasiliano Hatua 5: Futa chini na piga kura kwa “MRADI WA MAWASILIANO YA VIJIJINI HUKO ZANZIBAR”. Upigaji kura unafungwa tarehe 31 Machi 2024.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili