Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, anatarajiwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia Machi kesho kutwa.
Makamu wa Rais ataondoka nchini kesho kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mkutano huo ulitatanguliwa na mikutano ya maandalizi ya ngazi za wataalam ambayo ilianza Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika kesho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu.
Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi